SALUM ASHUSHA NEEMA KWA WALEMAVU MKURANGA.

Na Shushu Joel,Mkuranga.

MDAU mkubwa wa maendeleo katika Mkoa wa Pwani Ahmed Salum ameshusha neema kubwa kwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali kwa lengo la kuwafanya walemavu hao kutimiza ndoto zao walizokuwa nazo hapo awali

Mdau wa maendeleo katika Mkoa wa Pwani Ndg Ahmed Salum akiteta jambo na moja wa walemavu ambae ni mwanafunzi kutokea kata ya Tengelea(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la kukabidhi vifaa hivyo Salum alisema kuwa kutoa ni moyo na wala sio utajiri kama wengi wanavyofikilia,pia tunapotoa sadaka kwa wenzetu Mungu anakuongezea kwa kile unachokitoa.

Aidha Mdau huyo wa maendeleo alisema kuwa amekuwa akivutiwa sana na utoaji wa misaada kwenye nyanja mbalimbali kwa jamii kwa kusudi tu la kusaidia jamii na serikali kwa ujumla kwani serikali ina mambo mengi na peke yake haiwezi kukamilisha hivyo kama wadau tunapaswa kumsaidia Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli.

Katibu Tarafa wilaya ya Mkuranga Clement Muya sambamba na mdau wa maendeleo Ahmed Salu na wengine wakimkabidhi magongo ya msaada kwa ajili ya kutembelea 

“Nimetoa baiskeli 10 za miguu mitatu kwa ajili ya walemavu hao kufika sehemu wanazokuwa wanakwenda kwa haraka,magongo 10 ya kutembelea na fimbo za kuwaongozea watu wenye ulemavu wa macho”Alisema Salum

Pia amewaomba watanzania wenzake popote pale walipo kujitolea kwa kila jambo hapo walipo kwani unapotoa Mungu anakuongezea Baraka nyingi na za kipekee hapa duniani kwani hata sisi ni walemavu watarajiwa kama sio leo basi kesho.

Katibu wa Chama cha watu wenye ulemavu wilaya ya Mkuranga Hassan Katundu akisalimiana na mdau wa maendeleo Bw, Ahmed Salum katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya watu wenye ulemavu(PICHA NA SHUSHU JOEL)


Naye Ramadhani Haji ni mmoja wa walemavu waliofanikiwa kusaidiwa Baiskeli ya miguu mitano alisema kuwa ilikuwa kama ndoto wakati naambiwa na Diwani wa kata yangu lakini kumbe ni kweli Mungu atukuzwe.

“Nilikuwa na changamoto kubwa sana kila nikifikia muda wa kwenda na kurudi shule kwani nimekuwa nikitumia muda mwingi njiani kutokana na kukosa usafiri lakini leo Kaka Ahmed Salum amejitolea kutusaidia hivyo kaokoa maisha yangu na taifa zima kutokana na kuwa sasa nitawai masomo kwa wakati”Alisema Haji

Baadhi ya baiskel zilizotolewa na Ahmed Salum 

Aidha aliongeza kuwa mtu unapokuwa mlemavu sio kwamba ndio mwisho wa maisha yako hii ni mitihani tu ya dunia hivyo walemavu wenzangu tusikate tamaa kwa sababu ya maumbile tuliyonayo kwani kuna siku tutaonekana tu na jamii kama ilivyotokea sasa.

Aliongeza kuwa kwa kitendo hiki kilichotokea kwetu walemavu ni vyema na sahihi serikali ya awamu ya tano ni ya mfano wake kwani utekelezaji umekuwa ni mkubwa sana kuliko maneno.

Katibu tarafa Clement Muya akimpongeza mdau wa maendeleo kwa jinsi anavyojitolea(NA SHUSHU JOEL)
Kwa upande wake Katibu tarafa wa Mkuranga Clement Muya akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo amempongeza mdau huyo wa maendeleo huku akisema mkuwa ni mtu wa kuigwa katika jamii yetu kwani amekuwa akityoa sana misaada katika Nyanja nyingi.

Hivyo amewataka wote waliopewa vifaa hivyo kuhakikisha wanavilinda ili viendelee kuwasaidia kama moja ya uhitaji wao.

Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la ugawaji wa vifaa vya walemavu toka kwa mdau wa maendeleo Ahmed Salum(NA SHUSHU JOEL)

Aidha alisema kuwa mdau Ahmed smefanikiwa kutoa vitu vingi na wala haviesabiki nah ii yote anasema ni hamasa kubwa aliyonayo kutoka klwa Rais Dkt Magufuli.

MWISHO

 

 

Post a Comment

0 Comments