MBUNGE BAGAMOYO ANUNUA GARI KUOKOA MAISHA YA WAGONJWA.

 Na Shushu Joel,Bagamoyo

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mh Mkenge akizungumza na wananchi(NA SHUSHU JOEL)


MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Muharamu Mklenge amesema kuwa, kukosekana kwa soko la zao la nanasi kunatokana na kutokununulika kwa juisi ya zao hilo.


Mkenge ametoa kauli hiyo katika Kijiji cha Mkenge, Kata ya Fukayosi jimboni hapa ambapo ameanza ziara ya kuwashukuru wana-Bagamoyo MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Muharamu Mkenge amesema kuwa, kukosekana kwa soko la zao la nanasi kunatokana na kutokununulika kwa juisi ya zao hilo.


Mkenge ametoa kauli hiyo katika Kijiji cha Mwavi Kata ya Fukayosi jimboni hapa, akiwa kwenye ziara yake ya kushukuru baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa Oktoba 28.

Mkenge amesema kuwa yeye anafanyakazi Kampuni ya Bahkresa ambapo anatengeneza juisi mbalimbali lakini zenye soko za embe na machungwa, huku akiwahamasisha kilimo cha miwa, miembe na mikorosho.


Awali mkazi wa Kijiji cha Mwavi akijitambulisha kwa jina la Mtoro Chomboko amesema kwamba wakazi wengi wa Mwavi na Kiwangwa wanajihusisha na kilimo cha zao hilo, ambapo amemuomba Mkenge awatafutie soko.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Vigwaza katani hapo Andrew Tozzo amezungumzia changamoto ya maji na umeme ambapo amesema kero hiyo imekuwa adha kwao.


MWISHO 

Post a Comment

0 Comments