NDAKI "UDHIBITI WA UVUVI HARAMU UTAKUWA SHIRIKISHI "

 Na Anita Balingilaki,Busega

Waziri wa mifugo na uvuvi Mashimba Ndaki amesema wizara hiyo imejipanga kuhakikisha udhibiti wa uvuvi harama unakuwa endelevu badala ya kuwa wa zima moto .

Ameyasema hayo akiwa ziarani mkoani Simiyu wakati akiongea kwa nyakati tofauti na viongozi wa chama ,  serikali na wananchi wilayani busega mkoani hapo na kuongeza kuwa uvuvi haramu hauna tija na serikali ina mkono mrefu itawakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akiwa sambamba na wakuu wa wilaya za mkoa wa Simiyu

Aidha ameongeza kuwa wizara hiyo itahakikisha  udhibiti wa uvuvi harama unakuwa shirikishi ambao utatoa  matokeo ya udhibiti na sio kuishia kukamata vifaa na wavuvi haramu huku akiongeza kuwa  lengo  kubwa la udhibiti huo ni kumaliza  tatizo hilo.


" tutashirikiana kuanzia ngazi zote lengo likiwa kuhakikisha tatizo la uvuvi haramu linakwisha ili tupate tija kwenye uvuvi ..tutadhibiti kwa kufuata taratibu na sheria za nchi ,hatimaye tupate malighafi za kutosha kwenye viwanda tuongeze pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla "alisema Ndaki.


Mbali na hivyo amesema  wizara hiyo imejipanga kutoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa huku akiongeza kuwa sekta ya mifugo na uvuvi ina rasilimali nyingi ambazo zikisimamiwa vizuri zitachangia pakubwa.

Aidha ameongeza kuwa hakuna sababu ya mfugaji  na mvuvi kuwa maskini wakati  anazalisha malighafi nyingi zinazohitajika kwenye viwanda hususan vya ndani.


Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa sekta ya mifugo na uvuvi kwa  mkoa Simiyu kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa huo, mhandisi Mashaka Luhamba amesema jumla ya shilingi 282,333,930 zimekusanywa kwenye halmashauri zote za sita mkoani hapo ambazo zimetokana maduhuli ya samaki na mazao yake kwa kutoza leseni ,ushuru na faini za makosa mbalimbali kwa mujibu wa sheria na kanuni za uvuvi .


Mbali na hilo  mhandisi Luhamba amezitaja changamoto kuwa ni pamoja na wavuvi kuvamiwa ziwani na kunyang'anywa mali zao (nyavu ,injini) na wakati mwingine kupoteza maisha, ukosefu wa vitendea kazi, uhaba wa watumishi wa sekta ya mifugo na uvuvi na uhaba wa maji na malisho wakati wa kiangazi.


Akijibu changamoto ya wavuvi kuvamiwa na kunyang'anywa mali na wengine kuuawa waziri Ndaki amesema serikali haitakubari kuona mtanzania anapoteza maisha.


" hatutokubari kuona mtanzania anapoteza maisha yaan mtu yupo ziwani anajitafutia kipato atokee mtu amvamie amuue hii haikubariki hata kidogo tutahakikisha tunawalinda wavuvi wetu ili waendelee kujitafutia kipato chao cha halali" alisema Ndaki.


Akijibu changamoto ya wavuvi kuvamiwa na kunyang'anywa mali na wengine kuuawa waziri Ndaki amesema serikali haitakubari kuona mtanzania anapoteza maisha.


" hatutokubari kuona mtanzania anapoteza maisha yaan mtu yupo ziwani anajitafutia kipato atokee mtu amvamie amuue hii haikubariki hata kidogo tutahakikisha tunawalinda wavuvi wetu ili waendelee kujitafutia kipato chao cha halali" alisema Ndaki.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza waziri wa Mifugo na Uvuvi

Nae mbunge wa jimbo la Busega Simon Songe amesema bado kuna changamoto nyingi  kwenye sekta  ya uvuvi huku akiitaja moja wapo kuwa ni tozo nyingi ambapo ametumia nafasi hiyo kuiomba serikali kuona namna ya kuzitatua.


Katika hatua nyingine baadhi ya wananchi wameiomba serikali iwasaidie kutokana na uwepo wa viboko wanaohatarisha maisha yao  wakati wa ufanyaji kazi zao (uvuvi) sambamba na watu wanaowavamia na kuwanyang'anya vitendea kazi na wengine kuhatarishiwa maisha yao

MWISHO

Post a Comment

1 Comments