NAIBU WAZIRI WA MALIASILI AWATAKA TFS KUENDANA NA KASI YA AWAMU YA TANO

Na Shushu Joel,Dar es salaam. 

Akizungumza na Viongozi Waandamizi wa TFS  katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya TFS Mpingo House jijini Dar es salaam terehe 31/12/2020,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mary Francis Masanja, amepongeza TFS kwa kujijengea taswira imara ya ukusanyaji mapato ndani ya miaka tisa tangu kuundwa kwake lakini ametoa wito kwa Watendaji hao kuja na mkakati utakaohakikishia nchi upatikanaji rndelevu wa Rasilimali za Misitu na Nyuki. 

Naibu Waziri wa Maliasili Merry Masanja akizungumza na wafanyakazi wa maliasili(NA SHUSHU JOEL)


"Lengo kuu la ziara yangu ya leo ni kuja kujifunza, kujua TFS inafanya nini, nafahamu kazi zinaendelea za upandaji miti na Uhifadhi wa Mazingira lakini hata uzalishaji mazao ya Nyuki,lakini je tuna mkakati gani wa kuhakikisha hizi Rasilimali zinakuwa endelevu kwa ajiri ya vizazi vya baadaye? Kwa hiyo nawaelekeza Wahifadhi kuja na mkakati utakaohakikishia nchi upatikanaji wa Rasilimali za Misitu na Nyuki "Mh Mary Masanja. 


Aidha Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii amehimiza Wahifadhi Kote nchini kufanya kazi kwa uadilifu, kutojihusisha na rushwa, kutoa elimu ya uhifadhi kwa Wananchi na kuzingatia zaidi kanuni na sheria za usimamizi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki katika kutekeleza majukumu yao. 

"Tufanye kazi kwa mjibu wa Sheria, ninyi Wahifadhi Waandamizi waelekezeni walio chini yenu waendelee kufanya kazi kwa uadilifu, washirikiane na Wananchi kuhifadhi misitu kwa kuzingatia sheria kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi inayosimamiwa na Serikali ya awamu ya Tano,na nashukuru kwamba Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii amenipa kusimamia TFS, kwa hiyo TFS itakuwa jicho langu "Mh Mary Masanja. 


Awali Naibu Kamishina wa Uhifadhi anayesimamia Huduma Saidizi Emmanuel Wilfred aliwasilisha andiko fupi kuhusu Muundo wa TFS, Majukumu ya TFS, Mgawanyo wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Nchini, Mgawanyo wa Rasilimali Watu ndani ya TFS na Mgawanyo wa vyanzo za utendaji lakini pia kubainisha mahitaji mbalimbali ya TFS ili kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi. 

Naye Naibu Kamishina wa Uhifadhi anayesimamia Masoko na Matumizi ya Rasilimali Mohamed Kilongo amemuomba Mheshimiwa Naibu Waziri aridhie kuwepo kwa utaratibu maalumu wa kuwasajiri wafanyabiashara wanaosafirisha Mkaa kwa Pikipiki na baiskeli ili kuimarisha udhibiti wa ukataji holela wa Rasilimali za Misitu ikiwa ni pamoja na kuyabaini maeneo wanapochukulia Mkaa huo.


Kwa upande wake Naibu Kamishina anayesimamia Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo ameshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri na kumhakikishia ushirikaono katika kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa katika kikao hicho. 


"Nikushukuru sana, wewe ni mama, tunaimani kubwa na wewe. Mama anapokosewa hufinya lakini mtoto akilia anambembeleza"Mbwambo.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mary Masanja amefanya ziara yake ya kwanza Makao makuu ya TFS tangu alipoteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuri kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mwishoni mwa Mwaka huu 2020.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments