VIGOGO 4 UVCCM WASIMAMISHWA UONGOZI


Na Shushu Joel,Mkuranga


BARAZA kuu la Jumiuya ya  Umoja wa Vijana Mkoa wa Pwani limewasimamisha uongozi viongozi wanne wa jumuiya hiyo kutoka wilaya ya Mkuranga kwa kosa la kuongoza maandamano ya kufomtaka katibu wa jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Pwani Samiha Said akifafanua jambo kwa wajumbe wa mkutano huo.(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza na wajumbe wa kikao hicho Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya Uvccm Mkoa wa Pwani Samiha Said alisema kuwa Jumuiya hii haitowafumbia macho wale wote wenye nia mbaya na jumuiya.

Alisema kuwa moja ya sababu iliyopelekea kusimamishwa kwa vijana hao ni maamuzi mabaya waliyoyachukua kwa ajili ya katibu wao huku wakijua kanuni za jumuiya ziko wazi,Hivyo Baraza tumekubaliana watu hao watupishe kwanza mpaka pale vikao vya juu vitakapo amua.

"Tumewasimamisha uongozi viongozi hao kutokana na utovu wa nidhamu wa hali ya juu waliouonyesha ndani ya jumuiya yetu"Alisema Samaha Mwenyekiti Uvccm Mkoa wa Pwani.

Aliongeza kuwa Vijana wengi wamekuwa wakitumika vibaya na wale wanaotaka madaraka hivyo sasa sie kama baraza tumeamua kuwasimamisha uongozi vijana hao wa wilaya ya Mkuranga kwa kosa kubwa la utovu wa nidhamu kwa viongozi wao.


Aidha Mwenyekiti huyo aliwataka waliosimamoshwa uongozi pia kukatazwa kujihusisha na shughuli za jumuiya hiyo kuwa ni Omari Mataka Mwenyekiti wa Uvccm kata,Abdallah Nunda katibu Uvccm kata, Rehema Kiuta Katibu wa Hamasa kata na Mosi Siri Katibu wa Uvccm kata wote kutoka wilaya ya Mkuranga.

Mjumbe wa Barza kuu la UVCCM Taifa Ramadhani Mlao 

Kwa Upande wake Mjumbe wa Baraza kuu Taifa kutokea Mkoa wa Pwani Ramadhani Mlao amebariki uamuzi huo uliofanywa na Baraza la vijana mkoa wa Pwani kutokana na kuwa jumuiya yetu ni jumuiya ya pekee na yenye nidhamu ya hali ya juu.

Aliongeza kuwa jumuiya inanguvu kuliko mtu yeyote yule hivyo kwa hawa vijana waliosimamishwa uongozi ni fundisho kubwa kwa kiongozi yeyote ndani ya jumuiya hii kujiona yeye anaweza kuliko mwingine. 

Aidha Mlao ametoa ushauri kwa vijana wa jumuiya hiyo kuwa ni wakati sasa wa vijana kujitambua na kuacha tabia ya kutumikishwa kama punda hivyo kila mmoja ajitafutie kipato chake binafsi ili kuondokana na tabia ovyo zinazofanywa na watu walio na nia ovu na jumuiya yetu.

Naye Mjumbe wa Baraza hilo kutoka wilaya ya Bagamoyo ambaye pia ni katibu hamasa Pendo Moreto amesifu hatua kali za kinidhamu zilizochukulia na baraza hilo huku akisisitiza kuwa vijana tujitambue. 

Alisema kuwa ni aibu kubwa kwa vijana wenzetu kuona wakipewa barua za kufutwa uongozi ndani ya Uvccm lakini ndio kanuni zetu na kila mmoja wetu anazitambua kanuni hizo.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments