VIJANA ACHENI KUTETELEKA TAIFA LINAWATEGEMEA

 

Na Shushu Joel

VIJANA wa chama cha mapinduzi(UVCCM) mkoa wa Pwani wametakiwa kutokuteteleka na jambo lolote lile kwani taifa linawategemea kwa nafasi kubwa vijana hao miaka ijayo.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akisisitiza jambo kwa vijana wa mkoa huo(NA SHUSHU JOEL)
Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi(CCM) mkoa wa Pwani Hawa Mchafu alipokuwa akizungumza na vijana wa mkoa huo kwenye baraza la vijana lililoketi kwa ajili ya kujua wapi jumuiya hiyo ilipo na wanakwenda wapi.

Mbunge huyo aliwataka vijana kuendelea kupiga kazi kwani wao ni mtaji mkubwa na unaotegemewa na asilimia kubwa na taifa hili kutokana na jinsi chama hicho kinavyowalea ili baadae waje kuwa viongozi wakubwa katika nchi yetu.

“Suala la kupata uongozi ni jambo la subra tu kwani hata mimi nimetokeaUvccm hivyo naamini penye nia pana njia kubwa ni kujitambua na kuendelea kuwa karibu na jamii zetu katika masuala ya maendeleo ya kijami” Alisema Mchafu.

Mbunge Hawa Mchafu kulia na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Pwani Samaha Said wakionyesha ishara ya dole kwa Vijana(NA SHUSHU JOEL)
Aidha alisema kuwa ni vyema sasa kila kijana aliye ndani ya chama cha mapinduzi(CCM) ahakikishe anajishughulisha na jambo lolote lile kwa ajili ya kujiongezea kipato chake binafsi kwani hii itatujengea kujiamini katika kazi zetu za kisiasi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja huo wa vijana mkoa wa Pwani Samaha Seif Said amempongeza Mbunge huyo kwa ushauri wake kwa vijana na Zaidi jambo la kuwataka vijana kujishughulisha ili kuondokana na kuwa tegemezi kutoka kwa viongozi wa kisiasa.

Hivyo Mwenyekiti huyo amewataka vijana kuzingatia maneno yaliyosemwa na mbunge huyo ili yawe kama funzo kwa vijana wengine hapa nchini.

Baadhi ya wajumbe wakisikiliza maneno ya mbunge wa Viti maalum Hawa Mchafu.

“Endapo vijana tukiwa na shughuli zetu za kufanya itakuwa ni nguzo kubwa kwetu kwani hata kitendo cha kuchukua fomu kwa ajili ya uongozi heshima itakuwepo kutokana na kujiweza kwakoi”Alisema Samaha.

Naye Mjumbe ambaye pia ni katibu wa Uvccm wilaya ya Rufiji Simba Mohamed amempongeza mbunge huyo kwa ushauri wake wa kuwataka vijana kujitegemra ili kuwa na uchumi wao binafsi.

Mbunge Hawa Mchafu akiteta jambo na Simba Mohamed mara baada ya kikao cha Baraza la umoja wa Vijana(NA SHUSHU JOEL)

Pia amewataka viongozi kuwasaidia Zaidi vijana wa ccm kwa kuwapatia mafunzo ya ujasliamali au sido ili waweze kujifunza na kuwa na uwezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali kwani hii itasaidia kuwaondoa vijana kwenye dimbwi la omba omba.

MWISHO

0717913670

 

 

Post a Comment

0 Comments