Na Shushu Joel,Dar
ASASI isiyo ya kiserikali ya The Asma Mwinyi Foundation imetoa misaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi ya Uhuru mchanganyiko iliyoko Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi hao kuweza kuendelea na masomo yao kwa vitendo kama ilivyo kawaida yao.
Mkurugenzi wa Asasi ya The Asma Mwinyi Foundation kulia akikabidhi kifaa cha kuandikia wanafunzi wenye ulemavu wa macho(NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza wakati
wa zoezi la kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Asasi hiyo Bi,Asma Mwinyi
alisema kuwa Asasi hiyo imekuwa ikipambana na utatuzi wa changamoto mbalimbali
katika mashule ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ili waweze kupata mahitaji
yao kama wanavyopata wengine katika uendelezaji wa elimu hapa nchini.
“Asasi yetu imejikita Zaidi kwenye kutoa misaada ya aina mbalimbali ikiwemo vifaa kama tulivyokabidhi leo kwa wanafunzi wa shule ya msingi uhuru ili kuwaondolea wanafunzi hao changamoto hizo”Alisema Mkurugenzi huyo wa Asasi hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wakiteta jambo na Mkurugenzi wa The Asma Mwinyi Foundation mara baada ya kukabidhi vifaa maalum vya kusomea na kuandikia kwa walemavu wa macho
Aidha aliongeza
kuwa changamoto ni nyingi na zote zinahitaji kutatuliwa ili wanafunzi hao nao
waweze kujisikia wanatendewa haki kama wengine lakini kupitia kwa Asasi yetu imefanikiwa kutoa vifaa
vinavyotumika kuandikia maneno ya Nukta Nundu kwa wanafunzi ambao ni walemavu
wa macho waliopo katika shule hiyo.
Mbali na
kutoa misaada hiyo Mkurugenzi huyo wa The Asma Mwinyi Foundation amewataka
wananchi walio na uwezo kuendelea kujitolea kwa wahitaji ili kuwapunguzia
mahitaji yanayowakabili ili kuisaidia serikali.
Kwa upande wake msimamizi wa wanafunzi wenye ulemavu katika shule hiyo Bw, Ahmed Abdallah ameipongeza Asasi hiyo kwa jinsi ambavyo imekuwa msaada mkubwa kwa shule hiyo kwani imekuwa ikijitolea mara kwa mara kwenye shule yetu.
Mkurugenzi wa Asasi ya The Asma Mwinyi Foundation akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ambao ni walevu wa viungo mbalimbali.(Picha na Shushu Joel)
Aliongeza
kuwa shule yetu ilikuwa na changamoto za vifaa vya wanafunzi kuandikia yaani
Nukta Nundu lakini kupitia Asasi ya The Asma Mwinyi Foundation tumepokea vifaa
30 hivyo msaada huu ni mkubwa sana kwa shule yetu.
Naye mmoja
wa wanafunzi wa shule hiyo Alphonce Wilbert ameishukuru Asasi hiyo kwa misaada
hiyo ya vifaa vya kuandikia kwani walikuwa na changamoto kubwa lakini Asasi ya
The Asma Mwinyi Foundation imekuwa msaada mkubwa kwetu kwani mahitaji yalikuwa
ni makubwa kwetu.
MWISHO
0 Comments