MATIBABU YA MAGONJWA YA KINA MAMA NA MTOTO WA JICHO KUTOLEWA BURE.

Na Shushu Joel,Kibaha

Kituo cha afya MEDWELL kilichoko halmashauri ya mji Kibaha mkoani Pwani kinatoa  huduma za bure za upasuaji wa mtoto wa jicho zaidi ya wagonjwa elfu mbili  (2,000)  katika kipindi cha mwaka jana na mwaka huu mwezi  januari 2021.

Huduma ya upasuaji  wa mtoto wa JICHO katika kituo hicho ikiendelea.


Pamoja na upasuaji huo  wa mtoto wa JIcho , pia kituo hicho kimeendesha zoezi maalumu la kutoa matibabu bure  na upimaji wa magonjwa ya akina mama ikiwa ni  pamoja na upimaji wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi.


Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho Bashiru Khaki   alisema kuwa kambi hiyo ni ya siku mbili ambapo walilenga kuhudumia wakina mama zaidi ya 1000 lakini walijitokeza ni zaidi ya 400 ambapo hata hivyo wote walipatiwa huduma hizo bila malipo.


"Wingi wa wakinamama waliojitokeza kupata vipimo na matibabu baada ya kutangaziwa kuna huduma hii ya  bila malipo limeonyesha picha kuwa kuna uhitaji mkubwa wa huduma za afya, hivyo tunajipanga kutoa huduma hizi mara kwa mara ili wananchi wawe na afya njema na waweze kufanya kazi na kuinua uchumi wa nchi, alisema, Khaki

Kwa upande wa huduma ya macho pamoja na upasuaji wa mtoto wa Jicho,  mkurugenzi huyo alisema huduma hiyo hutolewa kilasiku ya jumatnne na ijuma na kuwa  siku zote hutolewa bure.


Naye Amina Ramadhani ni meneja rasilimali watu, alisema kuwa  zoezi hilo lilipangwa kufanyika kwa muda wa siku moja lakini kutokana na wingi wa wagonjwa litafanyika Siku mbili , jumamos na jumapili kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma za kutambua Afya zao.


" Medwel tumejikita zaidi kuhudumia jamii hususani katika suala zima la afya, hapa tunatoa huduma za vipimo mbalimbali ,xray na ultrasound, pia upasuaji , huduma za kulaza wagonjwa na nyingine nyingi, pia tunachimba visima na hata katika suala la elimu pia tunachangia, lengo ni kuisaidia serikali yetu katika kuimarisha afya ya wananchi wake," alisema Amina


Kwa upande wake Mganga mkuu wa mkoa wa Pwani Dr. Gunini Kamba  amekipongeza kituo hicho kwa jinsi kinavyounga mkono juhudi za  serikali katika suala la afya kwa wananchi wake na kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao pia amewataka  wadau wengine wa afya wajitokeze kufanya huduma kama hizo ili kurahisisha huduma za utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi wetu.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments