Na Shushu Joel,Chalinze
Halmashauri ya wilaya ya Chalinze hivi karibuni imeziwezesha timu za mpira wa miguu zinazoendelea na mashindano ya mpira wa miguu daraja la tatu,Timu zilizowezeshwa ni Msata United na Chalinze United.
![]() |
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Chalinze wakiongozwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ramadhani Possi Mwenye kaunda suti(NA SHUSHU JOEL) |
Timu hizo zimewezeshwa kila moja kiasi cha fedha za kitanzania Milioni moja(1,000,000/=), Fedha hizo zilikabidhiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mheshimiwa Geoffrey Kamugisha katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji akiwa na Watendaji wa Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bwana Ramadhani Possi.
Katika zoezi la makabidhiano ya fedha hizo walihudhuria waheshimiwa Madiwani wa kata ya Msata, Bwilingu na Pera pamoja na viongozi wa timu zote mbili yaani Msata United na Chalinze United.
Katika Hotuba yake ya kukabidhi fedha hizo Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Geoffrey Kamugisha aliwataka wanamichezo kushiriki katika mashindano kwa umakini wa hali ya juu ili kuweza kuitangaza Halmashauri katika sekta ya michezo hapa nchini,"Tuna kila sababu ya kuwa na Timu imara ya Halmashauri ya Chalinze na ikafanya vizuri katika mashindano ya michezo,hivyo nawatakia kila la kheri katika mashindano ya kumpata mshindi wa mkoa."Kamugisha alisema.
![]() |
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo akisisitiza jambo |
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Bwana Ramadhani Possi aliwataka viongozi wa timu kwa kushirikiana na Afisa Michezo wa Halmashauri kuweka mazingira ya Halmashauri ya Chalinze kumiliki timu ya Michezo itakayo wafanya vijana kujiajiri wenyewe kwa ujuzi walionao.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Msata Mheshimiwa Selestini Semiono kwa niaba ya madiwani wenzake aliishukuru Halmashauri ya Chalinze kwa kuona umuhimu wa Michezo katika Jamii na kuzichangia timu hizi mbili ili kusukuma gurudumu la Michezo katika Halmashauri ya Chalinze.
MWISHO
0 Comments