WANANCHI BUSEGA WAMFANANISHA SONGE NA RAIS DKT MAGUFULI KWA UCHAPAKAZI WAKE

Na Shushu Joel,Busega


WANANCHI wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu wamemfananisha Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Simon Songe na Rais wa Jamhuri ya Muungono wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na utendaji wake wa kazi.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Nyamikoma wakimzonga zonga Mbunge wa Jimbo hilo Mh.Simon Songe mara baada ya mkutano.(NA SHUSHU JOEL)
Wakizungumza mara baada ya mkutano wa hadhara uliofanywa na Mbunge huyo kwenye kijiji cha Nyamikoma B kata ya Kabita wananchi hao walidai kuwa utendaji,uwajibikaji na utekelezaji wa ufanisi wa kazi umekuwa ni kama wa Rais Magufuli kwa wanyonge wa Busega.


Malimi Sega ni mmoja wa wakazi wa eneo hilo alisema kuwa Mhe. Songe amekuwa kiongozi wa mfano kwetu kwani amekuwa msaada mkubwa kwa jamii na hasa katika kusukuma gurudumu la Maendeleo.

Umati wa wananchi wakiwa na Mbunge wao Mh.Simon Songe(NA SHUSHU JOEL)

"Leo tu amekutana na mama Mlemavu ambaye alionyesha huruma zake na kumchangia pesa kwa ajili ya kumsaidia ili kuhakikisha usafiri wake una kuwa wa uhakika kwa pale anapokuwa anahitaji kwenda"Alisema Sega.


Naye Masaganya Thomas amemsifu Mbunge huyo kwa jinsi ambavyo amekuwa na uchungu wa Maendeleo dhidi ya wanabusega wanyonge.


Aidha aliongeza kuwa kwa mwenendo huu wa Mh Songe tunaamini atafika mbali sana katika siasa ya maendeleo .

Moja ya majengo ya shule ya sekondari Venance Mabeyo.

Kwa upande wake Mbunge Mhe. SimonSonge alisema kuwa ziara yake itaendelea katika jimbo zima kutokana na kuwa na utaratibu wa kuwasikiliza wananchi.


Aliongeza kuwa shule yetu ya Venance  Mabeyo jnaendelea vizuri na muda wowote ule mambo yanaweza kuiva Hivyo Wazazi wezangu hakuna mtoto wa kukaa nyumbani kwa kisingizio chochote kile kwani serikali ya awamu ya Tano chini ya Dkt Magufuli imejithatiti kwa kila Jambo.

"Leo nimefanikiwa kutoa saruji mifuko 20 na milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa maabara na mambo mengi ili kuhakikisha shule hiyo ya Venance Mabeyo inakamilika. 

MWISHO

Post a Comment

0 Comments