Na Shushu Joel,Mkuranga.
MKUU wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Filberto Sanga ameukamata mtandao wa utapeli wa Ardhi unaendeshwa na genge la watu wahuni kwa kuwatapeli wananchi mbalimbali kwa madai kuwa wao wanauza eneo hilo la serikali.
Mkuu wa wilaya yua Mkuranga Filberto Sanga akiangalia nyaeaka za ofisi hiyo mara baada ya kuingia na kukagua na kujionea wizi mkubwa unaofanywa na watu hao.(NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza
katika ofisi hiyo ya matapeli hao Sanga alisema kuwa watu hawa wamekuwa
wakiwadanganya wananchi kuwa wilaya ya Mkuranga ina maeneo yanauzwa na hivyo
wananchi wengi wamekuwa wakija mkuranga na watu hao na kuwaonyesha eneo ambalo
ni mali ya serikali,kitu ambacho ni cha ajabu sana.
“Tumefanikiwa
kuwakata watu hao na taratibu za kisheria zinaendelea ili kujua walipata wapi
mamlaka ya kuuza kwa kuwatapeli wananchi hao” Alisema Sanga.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewatahadhalisha wananchi na hasa wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa tukio hilo la kutapeliwa na watu hao ambao hata jina la ofisi hawana.
Mkuu wa wilaya ya Mkururanga Filberto Sanga akipata maelekezo kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao walinunua viwanja kwa watu hao
Pia
aliongeza kuwa kwa kuwa jambo hili lipo polisi kwa sasa ni vyema wananchi wote
wakatambua kuwa hakuna kiongozi ambaye anakataa watu kujenga mkuranga wakitokea
Dar es Salaam ila cha msingi watu wafuate utaratibu wa mauziano kwani matapeli
wamekuwa wakiwadanganya sana wananchi huku serikali ya awamu ya tano chini ya
Rais Dkt Magufuli imekuwa ikiwakata na kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria.
Kwa upande wake mmoja wa wateja waliofanikiwa kukutwa kwenye ofisi hiyo na mwandishi wa habari hii alisema kuwa amekuwa akitoa pesa mara kwa mara lakini hakuna mafanikio yeyeote huku ahadi za kupelekwa kwenye maeneo zikiwa nyingi na zenye kupigwa tarehe kila siku. Hivyo kukamatwa kwa watu hawa kumetusaidia sana sisi wananchi tuliotapeliwa,
Aidha
amemuomba Mkuu wa wilaya hiyo kuendelea kuufuatilia mtandao huo uenda wakabaini
mambo mengi.
MWISHO
0 Comments