Julieth Ngarabali, Kibaha
Wakazi wa Kata ya Soga Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani wamedai wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kwakuwa wanalazimika kunywa maji ya kisima ambayo wamesema kuwa si salama kwa Matumizi ya binadamu kulingana na mazingira yalivyo.
Hayo yamebainishwa na wakazi hao kwenye ziara ya mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoani Pwani Michael Mwakamo alipofika Kwenye Kata hiyo kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili wakazi hao ambaye awali alitembelea Kituo cha DAWASA Mlandizi Ili kujionea hatua mbalimbali za usambazaji maji kwa wateja.
Kwa mujibu wa wakazi hao walidai kuwa tayari wameshaanza kupata madharambalimbali kiafya kwa kuugua homa za matumbo taifodi huku wakiamini kuwa chanzo cha kupata matatizo hayo ni maji wanayotumia.
"Mpaka sasa ni zaidi ya mwezi mmoja umepita mabomba ya DAWASA hayatoi maji lakini hatujui Sababu ni nini hivyo tunalazimika kunywa maji ya kisima ambayo kimsingi si Salma lakini tunalazimika kufanya hivyo kwakuwa tumekosa maji safi ya kunywa"alisema. Pili Mgaya
Kwa upande wake Fatima Saidi alisema kuwa tangu alipoanza kutumia maji hayo amekuwa akisumbuliwa na kuumwa tumbo hali ambayo kimsingi inamuathiri kiafaya na kiuchumi kwani amekuwa akitumia sehemu ya pesa zake kwaajili ya dawa na kuomba Mamlaka zinazohusika kufanya jitihada za kurejesha huduma hiyo Ili kuwaondolea adha wanayoipata.
Awali Mtendaji Mkuu wa DAWASA Cyprian Luhemeja akielezea mikakati ya kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa Wilaya ya Kibaha alisema kuwa hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu maeneo yote ya Mlandizi yatakuwa na huduma ya maji wakati wote.
Alisema kuwa ujenzi wa miradi ya maji unaendelea kutekelezwa kwa wakati hivyo maeneo yote yaliyokuwa na changamoto ya huduma ya maji hali hiyo haitajitokeza baada ya mwezi huo wa Desemba bali Wananchi wote wataendelea kupata huduma hiyo muhimu kwa uhakika.
"Tunaleta mabomba kwa wingi na Vijana watakaofanyakazi hiyo ni wa hapa maeneo ya jirani hivyo nieaombe wajiandae na shughuli ya kuchimba mitaro ya kusambaza mabomba ya maji"aliaema
Akizungumzia hali hiyo Mbunge wa Jimbo hilo Michael Mwakamo alisema kuwa ataenda kushauriana na watumishi wa DAWASA Ili kufanya jitihada za kurejesha huduma ya maji kwenye Kijiji hicho.
Mwiaho
0 Comments