KIBAHA WAANZA UKAGUZI KWA WASIO NA NA VYOO ILI KUEPUKA MAGONJWA YA MILIPUKO

 Na Julieth Ngarabali

Kibaha. Kamati ya Mazingira mtaa wa Tangini mjini Kibaha imeanza kukagua wananchi ambao hawana vyoo bora pamoja na kudhibiti utupaji taka ovyo ili,kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Baadhi ya takataka zikiwa zimetupwa ovyo eneo la jamaika kama zilivyokutwa na mpiga picha wetu

Mwenyekiti wa mtaa huo ,Shauri Yombayomba amesema hayo akiongea na waandishi wa habari kuhusu mpango wao wa kudhibiti milipuko ya magonjwa mjini humo.


Shauri amesema kamati hiyo imeanza kazi mapema mwezi huu kwa kutembelea nyumba hadi nyumba na kukagua hali ya vyoo na namna ya utunzaji wa mazingira .


Amesema katika ukaguzi  kamati hiyo ilibaini uwepo wa tundu moja la choo kwenye nyumba yenye wapangaji zaidi ya familia kumi hali ambayo ni ya hatari, lakini pia utiririshaji wa maji machafu kwenye eneo ambalo si salama kwa wananchi 


" Kamati hii pia imebainj baadhi ya kaya kutokuwa na vyoo, na pia wapo wafugaji wadogo wadogo wanatirisha maji kwenye makazi ya watu hali ambayo ni ya hatari kwani inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa ikiwemo kipindupindu" alisema Shauri.


Alisema, wananchi ambao wamebainika kuwa katika hatari ya kusababisha kero na matishio ya kuzusha maginjwa ya mlipuko katika mtaa huo wameitwa na kuonywa na kuingia mkataba wa kurekebisha kasoro hizo.


Kuhusu baadhi  ya wanakazi  waliokaidi wito wa barua wataitwa tena na wasipotokea hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao  ili kuweka mazingira safi katika mtaa huo, na kwamba kamati ya mazungira inaendelea kuzunguka katika mtaa huo nyumba hadi nyumba na kukagua maeneo ya kuhifadhia takataka.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Mariamu Saidi ameomba Serikali iwe inafanya ukaguzi wa kushtukiza mara kwa mara kwenye maeneo yao ili wanaotoririsha maji machafu waendelee kuchukuliwa hatua kwani  wanaharibu mazingira kwa kulet harufu mbaya na tishio la mqonjwa ya kuhara, kutapika na matumbo.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments