Na Mwandishi wetu.
NAIBU Waziri wa ardhi nyumba na makazi Dr. Angelina Mabula amewaagiza watendaji wa ardhi wa Mkoani Pwani kuwachukulia hatua kampuni zinazojishughulisha na urasimishaji ardhi kwani wamebaini baadhi ya kampuni hizo hazina mitaji zinategemea pesa za wananchi kuendesha shughuli hizo
Ameongeza kuwa kurejesha pesa za wananchi ilikuondoa malalamiko ya wananchi au kuchukuliwa hatua kali ili kuondoa hiyo kero ambayo imekuwa ni tatizo .
![]() |
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi Dr, Angellina Mabula akifafanua Jambo. |
Haya ameyasema wakati akiongea na Viongozi wa Halmashauri zote za Mkoani Pwani wakurugenzi pamoja na watendaji wa ardhi kwenye ukumbi wa mkutano wa mkuu wa Mkoa pwani.
Sambamba na hayo akawagiza Tena watendaji wa ardhi kutoka na kufuatilia maeneo ya serikali ambayo hayajapimwa wahakikishe wanayapima ili kuondoa migogoro na wananchi ambao wanayavamia.
Sambamba na hayo akatumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Bagamoyo kwa kazi nzuri aliifanya na kutambua na kutengapesa kwa ajili
Na baadae aligawa hati kwa kwa wananchi waliokuwa wamejitokeza kwenye mkutano huo wa Naibu Waziri huyo.
MWISHO
0 Comments