Na Shushu Joel
![]() |
Viongozi wa CCM Mkoa wa Pwani wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete huku akiwa ameshika Nishani aliyokabidhiwa na viongozi hao. |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kimemkabidhi cheti cha pongezi kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita(10) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la kukabidhiwa kwa Nishani hiyo Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno alisema kuwa kukabidhiwa kwa nishati huyo Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Kikwete ni.kutokana na juhudi na.msaada wake mkubwa kwa Mkoa wa Pwani katika masuala mbalimbali ya chama hicho.
Kwa upande wake Kada wa chama hicho Ahmed Salum ameipongeza ccm kwa kutambua mchango mkubwa uliofanywa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na hata kumtunuku Nishani ya heshima kwa kiongozi huyo.
Aidha Ahmed ameusifu uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani kwa kutambua thamani kubwa inayofanywa na viongozi na Makada kwa kuwapatia Nishani Mbalimbali za.ushiriki wao dhidi ya chama.
"Nimefurahia sana kuona Rais Mstaafu wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Nishani hii inaonyesha kuna siku hata mimi chama kitanipatia Nishani ya heshima kwa jinsi ninavyokipenda"Alisema Ahmed .
Pia Ahamed amewataka wananchi na wanaccm kuwaiga viongozi wetu waliomaliza kututumikia na wale ambao wako madarakani kwa jinsi ambavyo wamekuwa msaada mkubwa kwa jamii.
Naye Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewashukuru viongozi wote wa ccm na kuwapongeza kwa kuona msaada wake alioufanya na hata kumkabidhi Nishani .
MWISHO
0 Comments