Na Shushu Joel,Bagamoyo
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Zainabu Kawawa katika kuunga mkono juhudi za kukuza sekta ya michezo ametoa sapoti kwa kuchangia kiasi cha shilingi laki tatu kwa kikosi cha timu ya soka ya Bagafriends ambayo ni mabingwa wa Mkoa wa Pwani katika michuano ya ligi daraja la tatu ambayo kwa sasa inajiandaa na kivumbi cha ligi ya mabingwa wa mikoa ngazi ya Taifa inayotarajia kuazna kutimua vumbi lake mwishoni mwa mwezi huu 2021.
Kawawa
ametoa mchango huo wakati alipokutana na viongozi mbali mbali wa mchezo wa soka
wa Wilaya ya Bagamoyo,viongozi pamoja na
wadau wengine wa michezo lengo ikiwa ni kukutana kwa ajili ajili ya
kujadli na kupanga mikakati ambayo itasaidia timu hiyo iweze kufanya vizuri
sambamba na kuchangisha fedha ambazo zitasaidia wachezaji katika kipindi cha
ligi hiyo ngazi ya Taifa.
Pia Kawawa
amewaomab wadau mbali mbali wa michezo katika Wilaya ya Bgamoyo pamoja na Pwani
kwa ujumla kushikamana kwa pamoja katika kuisaidia kwa hali na mali timu hiyo
ili iweze kutimiza malengo yake yakuweza kufanya vizuri katika ligi hiyo na
kupanda daraja katika msimu unaokuja.
“Hii ni timu
yetu ya Bagafriends kwa hiyo mimi kaka mkuu wa Wilaya ninawaomba wadau wa
mchezo wa soka ndani ya Bgamoyo pamoja na Mkoa wa ujumla tushikamane kwa pamoja
kwa ajili ya kuipa sapoti ya kuisaidia michango mbali mbali ili wachezaji ambao
wanaunda timu hii waweze kucheza kwa molali zaidi na kutuwakilisha vema katika
michuano ya ngazi ya Taifa,”alifafanua Kawawa.
Kadhalika aliwaasa viongozi wa mpira wa soka katika Wilaya ya Bagamoyo kuweka mipango kabambe ya ambayo itaweza kufanikisha kupatika kwa ushindi wa timu hiyo ya Bagafriends lengo ikiwa ni kufanya vizuri zaidi katika michuano hiyo ya ngazi ya Taifa na kuongeza kuwa kwa sasa timu hiyo inatakiwa mahitaji mbali mbali ya msingi ikiwemo vifaa, fedha, mipira pamoja mambo mengine.
Aidha
aliwataka wachezaji wote ambao wanaunda timu hiyo ya Bagafriends kuwa na bidii
katika michezo yote na kuwa na nidhamu ya mchezo pindi wanapokuwa uwanjani na
kuzingatia sheria zote 17 za mchezo wa soka na kwamba ataendelea kuwapa sapoti
mbali mbali kutoka kwake ili kuweza kutmiza malengo amabyo wamejiwekea.
“Hii timu
kwa sasa ndio wawakilishi pekee wa Mkoa wa Pwani katika ngazi ya Taifa kwa hivyo hatuna budu wote kwa
pamoja tukawa kitu kimoja bila kujali timu imetokea sehemu gani lakini tutambue
kwamba ndio inauwakilisha Mkoa lakini mimi nina imani tukishikamana kwa pamoja
tutaweza kuleta mabadiliko zaidi katika Nyanja ya mchezo wa soko,”alisema
Kawawa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni aliwaomba wadau mbali mbali wa mchezo wa soka katika Wilaya ya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kuungana kwa pamoja kuichangia timu hiyo ya Bagafriends ili iweze kufanya vizuri katika michuano hiyo ya michuano ya mabingwa ngazi ya Taifa.
MWISHO.
0 Comments