Na Shushu
Joel
JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Pwani wamefurahishwa na utendaji kazi uliotukuka wa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bi Farida Mgomi.
![]() |
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Farida Mgomi akiongoza wajumbe na wanachana wa chama cha mapinduzi kuchimba msingi wa shule ya Sekondari katika wilaya ya Mkuranga(NA SHUSHU JOEL) |
Wakizungumza kwa wakati tofauti tofauti baadhi ya wanawake Mkoa huo walima kuwa tangu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti Mgomi amekuwa msaada mkubwa na kimbilio la wanawake katika jumuiya hiyo.
Mwajuma Ally
ni mkazi wa Kisemvule mara baada ya kuhojiwa na Mwandishi wa HABARI MPYA BLOG
alisema kuwa awali jumuiya hii ilionekana kama vile imekufa katika mkoa wetu
lakini tangu kuongoza kwa Farida Mgomi
kumekuwa na mabadiliko makubwa katika Nyanja za kimaendeleo ndani nan je ya
jumuiya hiyo
Aliongeza
kuwa Mwenyekiti amekuwa msaada mkubwa katika jamii na hasa katika mahusiano ya
jumuiya na wananchi mbalimbali yamekuwa yakizidi kuimalika siku hadi siku.
“Nakumbuka
kipindi cha kampeni cha chama chetu kilipokuwa kikisaka dola Mgomi akulala kwa
kuhakikisha waliokuwa wagombea wa chama chetu wanashida na hili lilifanikiwa
kwa asilimia mia”Alisema
Kwa upande
wake Habibu Khaji amesifu utendaji wa Mwenyekiti huo kwani amekuwa akijitolea
ku;liko wenyeviti wote ambao wamefanya kazi ya nafasi hiyo kwenye Mkoa wa
Pwani.
Hivyo amemtaka Mgomi kuendelea kufanya kazi za jumuiya kwa kuwatetea wanyonge ambao ndio wenye jumuiya yao.
![]() |
Farida Mgomi Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani akipiga chepe kutoa mchanga kwa ajili ya ujenzi wa moja ya shule za Sekondari katika kata ya vikindu wilaya ya Mkuranga(NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza
kwa njia ya simu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo (UWT) Farida Mgomi alisema kuwa
watu ndio wanaoona juhudi zake za utendaji wa kazi hivyo wanahaki ya kusema kwa
kile wanachofanyiwa na viongozi wao.
“Jumuiya
imekuwa ikifanya kazi mbalimbali za kijamii nah ii ni kutokana na kutokukaa
ofisini na sasa tunawafuata wanyonge walipo tupo”Alisema Mgomi.
MWISHO
0 Comments