Na Shushu Joel,Singida
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC) kufanya utafiti kuangalia namna ya kudhibiti kuongezeka kwa kina cha maji ya maziwa mkoani Singida.
![]() |
| Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara akizungumza na viongozi mbalimbali kutoka wilaya ya Singida mara baada ya kuwasili Mkoani humo.(NA SHUSHU JOEL) |
Ameliagiza
Baraza hilo kufanya tathmini na kutoa suluhisho la kuongezeka kwa kina cha maji
katika Ziwa Masogweda na Mulya katika manispaa na wilaya ya Singida ambayo
yamefurika na kuleta madhara katika makazi na mashamba.
Waitara alitoa agizo hilo jana wakati wa ziara ya kikazi mkoani humo baada ya kupata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Paskasi Muragiri ambaye aliomba zichukuliwe hatua kukabiliana na hali hiyo.
Muragiri
alisema ziwa hilo huenda likazingira vijiji hivyo viwili na kusababisha madhara
kwa wakazi wanaoishi humo hivyo alitumia nafasi hiyo kumuomba Naibu Naibu
Waziri huyo kulifanyia kazi suala hiyo katika ngazi ya kitaifa.
Katika ziara
hiyo pamoja na mambo mengine Waitara alitembelea machinjio katika manispaa hiyo
na kuitaka halmashauri hiyo kuharakisha mpango wa kuihamishia eneo lingine
walilotenga.
“Niwapongeze viongozi wa manispaa ya Singida nimesikia hapa mna mpango wa kujenga machinjo nyingine kwani baada ya hii na nina imani itakuwa ya kisasa na itakidhi mahitaji maana sasa hivi ninyi ni manispaa na mnahitaji eneo kubwa kuliko hili,” alisema.
![]() |
Pia katika
ziara hiyo alitembelea soko kuu na kuridhishwa na hali ya miundombinu ya
kuhifadhi taka ngumu pamoja na dampo lililopo katika eneo la Manga nje kidogo
ya manispaa hiyo.
Akizungumza
katika kikao na maafisa mazingira kutoka manispaa hiyo Waitara alisema ipo haya
ya kuwashirikisha wananchi katika maeneo yao katika masuala ya kuhifadhi
mazingira ili kupata taarifa kutoka kwenye vijiji ngazi ya chini.
Naibu Waziri
Waitara yuko katika ziara mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa
Sheria ya Mazingra ya mwaka 2004 na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira
hususan upandaji na utunzaji wa miti kwa kila halmashauri
MWISHO



0 Comments