SERIKALI KUMALIZA CHANGAMOTO YA VITAMBULISHO VYA TAIFA:WAZIRI SIMBACHAWENE .

Na Shushu Joel,Kibaha.


WAZIRI wa Mambo ya ndani Mhe. George Simbachawene amewahakikishia wananchi kuwa serikali imesha maliza tatizo la vitambulisho vya Taifa kwa wale wote ambao bado walikuwa hawajapata vitambulisho vyao.

Waziri wa Mambo ya ndani George Simbachawene kushoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(NA SHUSHU JOEL)

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani mara baada ya kufanya ziara kwenye ofisi ya mamlaka hiyo ya vitambulisho vya Taifa(NIDA).

Aliongeza kuwa ujio wa mashine mpya za uzalishaji wa vitambulisho hivyo zimeongeza tija kwa ongezeko kubwa la uzalishaji ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.


"Hizi mashine tulizozifunga hapa kibaha zinakasi kubwa sana ya uzalishaji kwani kwa saa inazalisha vitambulisho 1000 hadi 1200 hivyo kwa masaa kumi na sita mashine hiyo inazalisha jumla ya vitambulisho 32,000 hadi 35,000"Alisema Waziri Simbachawene.


Aidha Waziri huyo wa Mambo ya ndani amempongeza Mkurugenzi wa taasisi hiyo kwa usimamizi hodari wa taasisi hiyo. 


Kwa upande wake Mkurugenzi wa vitambulisho vya Taifa(NIDA) Dkt Anorld Kihaule amewahakikishia wananchi kuwa vitambulisho vitamfikia kila mwananchi popote pale walipo. 


Pia amewakumbusha wananchi kuvitunza vitambulisho vyao pindi watakapovipata kwani vitambulisho hivyo vitakuwa vinatumika sehemu mbalimbali.


Naye Mwajuma Ally(47) mara baada ya.kuhojiwa na waandishi wa habari alisema kuwa pindi vitambulisho hivyo vitakapoanza kusambazwa kwa wananchi vitakuwa msaada mkubwa kwenye masuala mbalimbali ya kitaifa. 


Aidha alisema kuwa kipindi kirefu walikuwa wakitumia namba tu za NIDA hivyo ujio wa hizi mashine zitakuwa msaada mkubwa kwa jamii.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments