Na Shushu Joel,Butiama
Mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini amepongeza na kutoa zawadi kwa shule za sekondari na walimu waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa taifa 2020 hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Butiama.
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Jumanne Sagini akimkabidhi zawadi mwalimu |
Mbunge Sagini amesema utoaji wa Tuzo kwa wanaofanya vizuri ni moja kati maazimio ya kikao cha elimu kilichofanyika 31, Desemba 2020, lengo likiwa kuwapa motisha walimu na wengine wasiopata wajifunze kuwa wakifanya vizuri katika taaluma na matokeo yakaonekana mamlaka inakutambua.
Zawadi zilizotolewa ni shilingi 150,000/= kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Chief Ihunyo baada ya kushika nafasi ya tano kati ya 19 kimkoa kwenye matokeo ya mtihani wa Taifa kidato cha sita. Huku zawadi ya shilingi 20,000/= zikitolewa kwa kila mwalimu aliyefanya vizuri shuleni hapo, ambao ni Kokugonza Banyikila wa Historia, Mabruki Issa wa Jiografia na Ndeshifose Nnko wa somo la kiswahili. Pia shule ya Wasichana ya Chief Wanzagi ilipata zawadi ya shilingi 150,000 baada ya kushika nafasi ya nne kimkoa kati ya 199 katika matokeo ya kidato cha nne, na shilingi 100,000/= imetolewa kwa Shule ya serikali ya Kukirango kwa kuoongoza kiwilaya kwa kushika nafasi ya 5 kati ya 23.
Shule zilizopanda kwa ufaulu mtihani wa taifa wa kidato cha nne nazo zilipata zawadi ya shilingi 50,000/= kila moja, ambazo ni Musoma Utalii nafasi ya 13 kati ya 199 Mkoa , Baranga ya 57 na Kiabakari kuwa ya 75. Huku kiasi cha shilingi 20,000/= kilitolewa kwa walimu waliofanya vizuri na kuingia katika shule 10 bora kimkoa mtihani wa Taifa kidato cha nne, walimu hao ni Amina Maingu wa somo la Kiswahili akishika namba moja kati 199 kimkoa na Jenester Nyonda wa Jografia akiwa nafasi ya tatu, wote wkitoka Shule ya Wasichana ya Chief Wanzagi.
Pia shilingi 30,000/= ilitolewa kwa kila mwalimu wa shule za serikali walioondoa alama F kwenye masomo yao ya mtihani wa Taifa kidato cha nne, ambao ni Zuberi Maregesi wa Kemia shule ya Kiabakari, Samwel Mandalu wa Kemia shule ya Bumangi na Benard Mwinuka wa somo la kiswahili shule ya Baranga. Zawadi nyingine ya shilingi 100,000/= ilitolewa kwa Shule ya Chief Wanzagi kutokana na kuwa ya kwanza kiwilaya kwenye mtihani wa Taifa wa kidato cha pili pia Shule ya Serikali ya Bumangi ikipata shilingi 100,000/= kwa kushika nafasi ya 5 kati ya 23 wilaya.
"Elimu ndio kipaumbele changu na cha Wanabutiama kwa sababu mtu akipata elimu changamoto nyingine zinajifuta na aliyesoma vizuri ni rahisi kutawala mazingira yake. Niwape pole walimu kwa changamoto za kutopanda madaraja na waliosababisha wanachukuliwa hatua, lakini hatuwezi kubaki kulalamikia madaraja badala yake tuwahudumie watoto wetu na taifa letu kiujumla kutokana nchi hii ipo uchumi wa kati itasadia elimu ndio itatupeleka viwango la juu zaidi," amebainisha Sagini
Naye Kaimu Afisa Elimu Sekondari Butiama Pendo Masalu ameeleza kuwa, matokeo ya mwaka 2019 hayakuwa mazuri kuliko ya 2020, kutokana na hali ya sasa wamepanda hatua zote kwani mtihani wa kidato cha sita wamepanda kwa asilimia 1.5, kidato cha nne asilimia 10.7 na kidato cha pili ni asimilia 9. Lakini lengo ni kupata asilimia 100. Endapo wakimtumia vyema muumini wa elimu ambaye ni mbunge.
![]() |
Asante kwa zawadi |
Aidha awali baadhi ya walimu walilalamimikia kutopandishwa kwa madaraja pia kutokuwepo mahusiano mazuri baina yao na watumishi wa Halmashauri pamoja na mazingira wlwanayoushi ndio chanzo cha matokeo mabaya. Ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Diana Sonno, alimshukuru mbunge kwa kwa njia anazotumia ili kuhakikisha hawako nyuma tena kielimu ikiwemo kujenga mahusiano mazuri na walimu.
"Ni kweli tangu mwaka 2017 walimu hawajapanda madaraja lakini sote tunatambua changamoto ilikuwa ni utawala, tunaendelea kuboresha huduma zetu halmashauri ili watumishi na wananchi wapate huduma stahiki na siyo
MWISHO
0 Comments