NA MWANDISHI WETU
JESHI la polisi mkoa wa Simiyu limemkamata mtu mmoja mwanamme mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Bunda mkoani Mara kwa kukutwa na KOBE 438 wenye thamani ya Sh 71,161,866 bila ya kuwa na kibali.
![]() |
Baadhi ya kobe wakiwa wamekamatwa |
Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu,Kamishina Msaidizi wa PolisACP)Richard Abwao amesema kuwa tukio la kukamatwa kwa mtu huyo lilitokea machi 21 mwaka huu majira ya saa 2.00 usiku katika eneo la Dutwa wilayani Bariadi.
Amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amewahifadhi KOBE hao katika mabegi matatu na kobe hao wamekabidhiwa katika idara ya Maliasili kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Kamanda Abwao amesema kuwa mtuhumiwa yuko mahabusu na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Aidha Kamanda Abwao ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa mkoa huo kujiepusha na vitendo vya kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Pia amewaomba wananchi kuendekea kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu katika maeneo ya makao yao ili kuufanya mkoa huo kuwa mahali salama kwa kuishi.
MWISHO
0 Comments