CHALINZE YAJIKITA KWENYE UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

Na Shushu Joel,Chalinze 


HALMASHAULI ya Chaljnze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani imejikita kwenye utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusudi la kuwapatia wananchi wepesi wa upatikanaji wa huduma.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete akifafanua jambo kwa mwenyekiti wa CCM Ramadhani Manebo( NA SHUSHU JOEL)


Akizungumza na Mwandishi wa habari wa HABARI MPYA MEDIA Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete alisema kuwa viongozi tumejikita kutatua changamoto za wananchi ambazo zilikuwa zikiwakabili na zile ambazo zimepangwa kutekelezeka ili zitoe huduma kwa jamii.


Aliongeza kuwa ujio wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoani umekuwa chachu ya maendeleo kwetu.


Aidha Kikwete ameupongeza uongozi wa CCM Mkoa uliokuwa ukiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa Ramadhani Maneno.


Pia Kikwete alisema kuwa viongozi hao wa CCM wamefanikiwa kuona miradi mbalimbali iluyojengwa kwa ushirikiano wa wananchi na serikali.

Picha ya pamoja ya viongozi wa Serikali na Chama mara baada ya ukaguzi wa miradi mbalimbali chalinze


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno ameipongeza chalinze kwa utekelezaji mkubwa wa ilani ya chama .


Aidha amewataka wakazi wa chalinze kuhakikisha wanakuwa mstali wa mbele katika kutunza miradi hiyo ili kutimiza majukumu yaliyopangiliwa matumizi ya miradi hiyo.


Naye Mnec wa Mkoa huo Haji  Jumaa amemsifu mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete kwa jinsi ambavyo amekuwa kiungo kikubwa baina ya wananchi na serikali na.hasa kwenye hamasa ya utekelezaji wa ilani ya CCM .


MWISHO

Post a Comment

0 Comments