Na Shushu Joel, Chalinze.
SERIKALI ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inaendelea na juhudi za kuhakikisha Vito vya Mama na Mtoto vinabaki historia.
| Viongozi wa halmashauri ya chalinze wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe, Ridhiwani Kikwete kukagua jengo la Mama na Mtoto(NA SHUSHU JOEL) |
Tangu kuingia madarakani kwa serikali hiyo chini ya Rais Dkt. John Magufuli miaka mitano iliyopita kunekuwepo na juhudi za makusudi za kuhakikisha vifo vinavyoikabili jamii hiyo inabaki historia.
Hayo yameelezwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waandishi wa habari katika hospitali hiyo akiambatana na Mkurugenzi wa halmashauri Ramadhani Possi, Diwani wa Kata ya Msoga Ramadhani Mwinyikondo, Ofisa Mipango Shaabani Milao na viongozi mbalimbali.
Ridhiwani alianza kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia halmashauri hiyo kiasi hicho cha fedha ambacho kimefanikisha ujenzi huo unaoendelea katika hospitali hiyo.
"Leo tumekuja kujionea mradi wa jengo la Mama na Mtoto linaloendelea kujengwa katika hospitali yetu ya Wilaya ya Msoga, ambapo inalenga kuunga mkono juhudi za serikali za kumaliza vifo vya mama na mtoto" alisema Ridhiwani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ramadhani Possi alisema kuwa kukamilika kwa jengo hilo kunakwenda kufunguza ukurasa mpya wa maendeleo katika sekta ya afya, kwani kutaondoa vifo kwa walengaa hao.
"Tunaishukuru Serikali yetu chini ya Rais wetu Dkt. John Magufuli kwa msaada mkubwa anaoendelea kutupatia katika nyanja mbalimbali, na leo hii tunashuhudia ujenzi wa jengo hili la Mama na Mtoto linaloendelea kujengwa katika hospitali yetu ya Msogo," alisema Possi.
0 Comments