MBUNGE KIBAHA VIJIJINI ATAKA MASHAMBA PORI YAFUTWE.

Na Shushu Joel,Kibaha.

MBUNGE wa jimbo la kibaha vijijini,wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Mhe.Michael Mwakamo ameitaka halmashauri yake kuhakikisha wanayaorodhesha mashamba pori yote yaliyo jimboni humo na kuandika mapendekezo ya kufutwa.

Mbunge wa Kibaha Vijijini Michael Mwakamo akisisitiza jambo kwa wananchi wa kata ya Soga(NA SHUSHU JOEL)

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msufini kata ya Soga wakati wa ziara ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hao.

Aliongeza kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi ya wananchi juu ya migogoro ya wakulima.na wafugaji huku chanzo kikubwa ni mashamba pori makubwa ambayo yametelekezwa na watu mbalimbali hali inayopelekea wafugaji kuingiza mifugo yao .


"Nimezungumza na Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Mhe William Lukuvu na kusema kuwa wao kama Wizara hawana shida bali wanachosubili ni mapendekezo tu kutoka halmashauri husika"Alisema Mwakamo.


Mbali na hilo Mbunge huyo amewataka wananchi kuendelea kuwa na subra kwani kuna mambo makubwa ya kimaendeleo ambayo miaka mingi walikuwa wanayatamani na yasifike.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Msufini kata ya Soga wakimsikiliza mbunge wao Michael Mwakamo kwa umakini.(NA SHUSHU JOEL)

"Mbunge wenu nimejipanga kuhakikisha tunapata mahitaji muhimu kama vile Maji,Umeme,Miundombinu ili viweze kuraisidha maisha yetu ya kila siku"Alisema.


Kwa upande wake Bi, Mariam Ndalawa(54) Mkazi wa kata ya Soga amempongeza mbunge kwa kutambua changamoto zinazowakabili wananchi wake  na hata kufikia hatua ya kupunguza changamoto ndogo ndogo.


Aidha aliongeza kuwa kukamilika kwa miradi ya maendeleo katika kata yetu kutasaidia kutatua changamoto  pia kufungua milango ya uwekezaji kwa wadau mbalimbali ambao watakuja kuwekeza katika kata yetu.


Naye Kaimu Mkurugenzi ambaye ni Afisa Mipango Bi,Beatha amemwakikishia Mbunge kuwa wao kama halmashauri watahakikishia wanafanya hivyo ili kuwasaidia wananchi wa Soga.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments