IMALAMATE YAFULIKA KUMLAKI SONGE.

Na Shushu Joel, Busega.

WANANCHI wa kata ya Imalamate iliyoko wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wamefulika kwa furaha shangwe na ndelemo.

Mbunge wa Jimbo la Busega Simon Songe akisalimia na moja wa wazee wa kata ya Imalamate(NA SHUSHU JOEL)

Wakizungumza mara baada ya kikao wakazi hao wa Imalamate wamempongeza Mbunge huyo kwa uchapaji kazi wake  kwa wanabusega.


Kulwa Stephano ni mkazi wa Imalamate alisema kuwa kipindi hiki cha uongozi wa Mbunge wetu Mhe. Simon Songe kata yetu imekuwa na mabadiliko makubwa katika maendeleo na hasa katika elimu,umeme,Afya  na miundombinu. 


Aliongeza kuwa ndani tu ya kipindi hiki tumepata misaada mingi kwa nguvu zake hivyo viongozi hawa kama kina Songe wanaposwa kutizamwa kwa jicho la tatu kutokana na upendo wake wa kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Aidha Kulwa amempongeza mbunge wa Jimbo hilo Mhe Songe kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni hamsini(50,000,000) kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati ya Ng'wang'wale iliyotelekezwa na viongozi wengi waliopita.

Naye Mwashi Malendeja(66) Mkazi wa kata hiyo ya Imalamate amemshukuru Mbunge Mhe Songe kwa juhudi zake za ufanikishaji wa maendeleo pia amekuwa msaada mkubwa kwetu kina Mama kutokana na kuwa maendeleo anayoyafanya yemekuwa yakitugusa kina mama moja kwa moja. 


Hivyo Mama huyo amemtaka  Mhe. Mbunge Songe kuhakikisha anapiga kazi zake za maendeleo bila uoga wa aina yeyote ile kwani watu wengi sasa tumeelika na kujua yupi ni kiongozi wa kweli katika kutufanikishia maendeleo yetu.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Simon Songe amewashukuru wananchi wa kata ya Imalamate na kuhakikishia maendeleo katika kata hiyo yanayokuja bila wasiwasi wowote ule.


Aidha Mhe Songe alisema kuwa kata ya Imalamate kuna shule mpya inakuja na tayari fedha serikali imekwisha kutolewa kiasi cha shilingi milioni 50 ,fedha ya kumalizia zahanati pia kuhusu barabara tumekwisha maliza.


Pia niwashukuru wananchi wa kata ya Imalamate kwa kuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha mnapata maendeleo kwa kuchangishana wenyewe na kuanzisha miradi mbalimbali.


MWISHO.

Post a Comment

0 Comments