SONGE AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO BUSEGA.

Na Shushu Joel,Busega.

Mbunge wa Jimbo la busega mhe Simon Songe akikabidhi mara tatu(NA SHUSHU JOEL)

MBUNGE wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu Mhe Simon Songe amemwaga vifaa vya Michezo katika jimbo hilo kwa ajili ya ligi inayotarajiwa kuanza kuchezwa hivi karibuni.


Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa hivyo Mbunge huyo amewataka vijana wa kila kata kujiandaa kwa mazoezi makali kwani ligi hiyo itakuwa ya pekee na yenye ushindani mkubwa kutokana na zawadi nono za washindi watakaoibuka kwenye ligi hiyo.


"Naamini kuwa kwenye Jimbo langu la Busega kuna vijana wenye vipaji vya kucheza mpira katika timu kubwa hapa nchi kama Simba,Yanga na Azam na hata Ulaya kikubwa ni jinsi ya upatikanaji wao"Alisema Songe.


Aidha aliongeza kuwa amewasiliana na viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini kwa kusudi la kutuma michuano hiyo ili kupata vijana ambao wanaweza kuja kuwa msaada mkubwa kwenye timu ya Taifa.


"Nakabidhi jezi hizi kwa kila Diwani wa kata ili yeye aweze kuwa mstali wa mbele katika kufanikisha upatikanaji wa timu ya kata ambayo itakuja kushiriki michuano hiyo ya Jimbo Cup"Alisema Songe.


Akipokea jezi hizo Diwani wa kata ya Nyashimo Micknes Mahela amempongeza mbunge huyo kwa kutengeneza ajira kwa vijana wa jimbo zima.


:Aidha amemtaka Mbunge huyo kuhakikisha anawasaidia vijana wenye vipaji "


Naye Mrisho Malima mmoja wa wachezaji wa mpira huo.wa miguu  amemponge Mbunge Songe kwa kuonyesha jinsi gani alivyo kwa jamii.


"Jezi hizi zinaonyesha jinsi gani alivyo na moyo wa mbele kwa 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments