Na Shushu Joel,Pwani
Mhe Abubakar Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ametembelea na kukagua Ujenzi wa Kiwanda cha kampuni ya Raddy fibre Solution, kiwanda hicho kinazalisha nyaya za Mkongo wa Mwasiliano Optic Fibre Cable.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza na mmoja wa viongozi wa juu wa kiwanda hicho mara baada ya kutembelea(NA SHUSHU JOEL) |
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani Kunenge amepongeza Uwekezaji huo wa kisasa na kusema kuysema kuwa kiwanda hicho kitafungua fursa kwa wananchi wa mkoa huo na hasa vijana
Pia amemtaka mkurugenzi wa kiwanda hicho kuhakikisha kuwa wanatumia vyombo vya habari ili kujitangaza na jamii ijue kile kinachofanyika katika kiwanda hich.
"Viwanda hivi lazima vifaamike, ni kiwanda muhimu kwa Nchi yetu".Alisema Kunenge
Amewaasaa wafanyakazi wanaofanya kazi hapo kujituma na kujifuza kwa bidii kwa kuwa ni fursa ya kupanua ujuzi wao katika ulimwengu wa sasa.
Kiwanda hicho kinachomilikiwa na wazawa kina Uwekezaji wa Bilioni Shiling 17, na uwezo wa Kuzalisha kilometa 24000 za Fibre cable, aidha kikikamilika kitatoa ajira za moja kwa moja 400.
MWISHO
0 Comments