"VIJANA ACHENI KUBWETEKA" ASEMA MBUNGE SABO

Na Shushu Joel Busega.


MBUNGE wa viti maalum kupitia kundi la Vijana (UVCCM) Mkoa wa Simiyu Lucy Sabo amewataka vijana wa wilaya ya Busega Mkoani Simiyu kutokubweteka na badala ya amewataka kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua katika maisha.

Mhe Mbunge wa vijana kupitia mkoa wa Simiyu Lucy Sabo akifafanua jambo kwa Baraza la vijana wa wilaya ya Busega(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) wilaya ya Busega Mhe Sabo  alisema kuwa Mkoa wa Simiyu una fursa nyingi ambazo zinaweza kufanywa na vijana hivyo vijana mnatakiwa kuchangamkia nafasi hizo kwa kuunda vikundi ili muweze kukopesheka kwa ajili ya kupata mtaji.

"Vijana wengi wamekuwa wakililia mitaji na ajira hivyo niwashauri kuunda vikundi na kuvisajili ili muweze kupata nafasi mbalimbali kwa ajili ya kupata tenda na zitawaingizia kipato"Alisema Sabo.

Aidha Mbunge huyo amewataka vijana kuendelea kudumisha mahusiano na viongozi wao na pia kuwasemea kwa mazuri wanayoyafanya ikiwemo Rais wetu Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Busega Donald Luge akisisitiza jambo kwa vijana(NA SHUSHU JOEL)

Kwa Upande Ngutu Laurence Mwenyekiti wa Uvccm kata ya Lamadi amempongeza Mbunge huyo kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa Jumuiya ya Umoja wa vijana (UVCCM) wilaya ya Busega katika utoaji wa fursa kwa vijana.

Aidha amewataka vijana kuendelea kunufaika na mbunge Mhe Sabo kwani msaada wake umekuwa mkubwa Bungeni kwa kuwatetea vijana wa Busega.

Naye Jesca Babasha amempongeza Mhe. Sabo kwa juhudi zake za kuunganisha Umoja wa vijana na hasa katika kuhakikisha vijana wanajikwamua katika hali zao walizonazo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments