NAIBU WAZIRI WA AFYA ATAKA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII KUJIKITA KWENYE MAFUNZO YA VITENDO.

 Na mwandishi wetu kutoka Mufindi Iringa.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Mwanaidi Ali Khamis amevishauri Vyuo vya maendeleo ya jamii nchini kujikita zaidi kwenye mafunzo ya vitendo ili wahitimu waweze kujiajiri badala ya kuhitimu na kusubiri ajira za serikali.

NAIBU Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto anayeshughulikia maendeleo ya jamii Mhe Mwanaidi Khakis wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja 


Naibu Waziri huyo ametoa ushauri huo leo Julay 7,2021 baada ya kukagua shughuli mbali mbali za ujasiriamali na kilimo cha parachichi zinazofanywa na wanachuo wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Rungemba kilichopo wilayani Mufindi.

"Ni vyema vyuo vyetu nchini kuanza kufundisha wanafunzi kwa vitendo ili wanapotoka hapa wanakuwa na ujuzi wa kukabiliana na maisha katika kilimo ufugaji na ujasiliamali kwani serikali haina uwezo wa kuajiri wahitimu wote nchini"


Mwanaidi  aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa jitihada zake za kuisaidia jamii inayowazunguka na kutaka kuongeza ubunifu kwa miradi zaidi na kuwasaidia wahitimu kubuni miradi kwa mawazo yao binafsi na kuyafanyia kazi.


Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Rungemba Kidubya Kulamiwa amesema uhamasishaji wa kilimo cha parachichi una lengo la kuongeza kipato cha wananchi ili wajikimu kimaisha na kujinusuru na janga la lishe duni na udumavu.


Kulamiwa ameongeza kuwa  kilimo cha zao la parapachichi kitawasaidia wananchi kuinua kipato chao pamoja na kudumisha afya za familia zao kwa kuzingatia mlo kamili na kutokomeza udumavu katika Mkoa wa Iringa.


"Tunawafundisha wanafunzi wetu ujasiliamali wa kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa ubunifu wao wenyewe pia tunajihusisha na upandaji Miche  ya zao la  parachichi ili kujinusuru na janga la udumavu na lishe duni kwasasa chuo kimepanda hekali  500,na tunatoa elimu ya upandaji miti,mafunzo ya chakula na lishe.

Kutokana na kunufaika na mafunzo kwa vitendo, wananchi wameiomba serikali kukipandisha  chuo hicho cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kuwa Chuo Kikuu.

Na kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM kata ya Rungemba  ndugu Jackson Mbenule  amasema  chuo kina ukubwa wa hekali 260 na chuo kinatoa stashahada pekee hivyo kwa ukubwa huu wa chuo hivyo wanaomba serikali ianze kutoa elimu ngazi ya shahada.

 Pia amemshukuru Naibu Waziri  kwa zawadi ya  vifaa vya kuvunia maparachichi  kwani vitawasaidia katika shughuli zao za uvunaji  na pia kwa upande wa vifaa vya kulinia asali watalina vizuri kwa sababu mwanzon walikuwa wanatumia njia za kienyeji ambazo sio rafiki.. 

Akiwa chuoni hapo, Naibu waziri huyo amezindua vyumba viwili vya madarasa  yatakayopunguza uhaba wa madarasa huku akiahidi kuitafutia ufumbuzi changamoto ya mabweni.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments