Na JULIETH NGARABALI
Ushirikiano uliopo baina ya wawekezaji wazawa na Serikali imeanza kuzaa matunda ambapo Kampuni ya kuunganisha magari ya BM Motors imeweza kuunganisha magari makubwa matatu ya kubebea abiria na kwamba tayari moja limeuzwa nchini Kongo.
Mkurugenzi wa BM Motors Jonas Nyagawa amesema hayo baada ya kupokea cheti cha udhibitisho wa viwango kutoka Shirika la viwango Tanzania (TBS) katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Shirika hilo Ubungo Dar esalaam jana.
Nyagawa amesema katika kiwanda chake kilichopo Zegereni Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani amefanikiwa kuunganisha mabasi ya abiria matatu na moja limeuzwa nchi za nje na mafanikio hayo yote ameyapata kwa muda mfupi tuu kwa sababu ya ushirikino mzuri uliopo kati yao na Serikali.
"Nashukuru kufikia hatu hii ya kupata cheti kutoka TBS na sasa magari yanayounganishwa na Kampuni ya BM yatajulikana kitaifa na kimataifa hivyo ninatarajia kupata soko kubwa , nimejipanga kwa uzalishaji wa kutosha maana najua nitapata wateja sasa"amesema Nyagawa.
Nyagawa alisema utaalamu ulitokana na yeye kujifunza kutoka kwa nchi ambazo zinafabya hivyo lengo kuokoa fedha za kununua mabasi ya abiria kutoka nje ya nchi.
Naye MKurugenzi mkuu wa TBS Yusuph Ngenya ameeleza kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Mei wameweza kutoa vyeti na leseni za kutumia alama ya TBS 246 kwa wateja wao.
Ngenya amewataka wajasiriamali na wawekezaji kuzingatia taratibu za bidhaa na vitu wanayozalisha kwa manufaa ya Taifa na pia kuendelea kuzalisha bidhaa zenye Ubora ili ziuzike kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mwisho.
0 Comments