RC KUNENGE AZINDUA KAMPENI YA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI PWANI

Na Shushu Joel,Kibaha

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Abubakar Kunenge amezindua Kampeni ya kushughulikia Migogoro ya  Sekta ya Ardhi Mkoani  Pwani. Katika Uzinduzi uliofanyika leo 13 Julai,2021  Mjini Kibaha amefanya Kikao na Uongozi wa Mkoa huo uliomshirikisha Mhe William Lukuvi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Kamati ya Usalama ya Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizunguza na watu mbalimbali waliojitokeza kwenye mpango huo wa kumaliza migogoro ya Ardhi.


Ameeleza kuwa watafanya ziara na Mhe Waziri wa Ardhi katika Wilaya za Kibaha, Bagamoyo, Mafia, Mkuranga, Rufiji na Kibiti kuanzia Tarehe 14 Julai,2021  hadi Tarehe 22 Julai 2021 kushughulikia na kutatua Migogoro ya Ardhi.


Kunenge, amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanatumia nafasi zao katika kutatua migogoro ya Ardhi.


Kunenge pia amewataka Viongozi hao wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaboresha Daftari la makazi na kuhakiki idadi ya mifungo iliyopo mkoani Pwani ili kuepukana na Migogoro ya Ardhi.

katika hatua Nyingine RC Kunenge amesema kuwa hatosita kumchukulia mtu hatua kali ya kisheria kwa yeyote yule atakaefanya uvamizi wa aina yeyote.

“Sheria zipo wazi  watu wanavamia lakini hawachakuliwi hatua, hivyo sasa tutachukua hatua  kali hatutaonea mtu ila tutatenda haki” alisema Kunenge

Pia amewataka viongozi hao kusimamia haki na kufanya kazi kama wanavyotakiwa”tumekuja Pwani  kufanya kazi tuhakikishe tunafanya kazi.

Naye Waziri Wa Ardhi Mh. Lukuvi kwa Upande wake amewataka Wakuu wa Wilaya  kuhakikisha wanatatua migogoro ya Ardhi na wasisubiri mpaka wananchi waje kulalamika kwa Viongozi wakuu,

Pia ameziagiza Halmashauri zote Tanzania kuhakikisha wanazisimamia hizi kampuni binafsi za upimaji wa ardhi na wasiziache zikafanya kazi zenyewe.


“Kampuni Binafsi lazima zisimamiwe na zisiachwe zifanye kazi zenyewe kwani msimamizi wa Ardhi katika Halmashauri ni Halmashauri” alisema Lukuvi.

mwisho

Post a Comment

0 Comments