Na Shushu Joel ,Busega.
CHAMA cha Maendeleo na Demakrasia kimempongeza Mbunge wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu Mhe Simon Songe kwa kuutafuna mfupa uliowashinda wengi wakati wa uongozi wao.
![]() |
| Mbunge wa jimbo la Busega Simon Songe Akimkabidhi saruji Diwani wa kata ya malili Christopher Bukalasha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari. |
Hayo yameelezwa na Diwani wa kata ya Malili Christopher Bukalasha wakati alipokuwa akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Gininiga kwenye ziara ya Mbunge huyu katika kata.hiyo ya malili
Alisema kuwa kata ya malili ilikuwa imesaulika kimaendeleo kwa muda wa miaka mingi lakini tangu Mhe Sknge awe Mbunge amekuwa msaada mkubwa kwa kata yetu ya malili.
"Kwa kweli tulisaulika sana katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo barabara ya kutoka malili kwenda kijiji cha Mwamigongwa ambapo palikuwa hapapitiki lakini sasa madaraja madogo manne yamewekwa na tayari mkandarasi tunamuona kwa ajili ya ujenzi wa barabara,nguzo za umeme na miradi mingine mingi ikitekelezwa"Alisema Bukalasha.
Mbali na hilo Diwani huyo amekishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa uono wake wa hali ya juu katika kufanya uteuzi wa Mbunge wa Jimbo la Busega ambaye sasa amezidi kuwa msaada mkubwa kwa wananchi ambao miaka mingi walikuwa na ndoto za kuwa na kiongozi wa aina kama hii.
Aidha amewataka wananchi wa kata zote za Jimbo la Busega kuhakikisha wanaishikilia tunu hii iliyodondoka kutoka kwa Mungu.
Kwa upande wake Malimi Izengo (67) Mkazi wa Kijiji cha Mwamigongwa amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Songe kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa jamii ya Mwamigongwa kwani tulikuwa tuko mwituni kwa kipindi kirefu.
"Tangu nizaliwe kwenye kijiji hiki na leo nimezeeka sikuwai kuwaza kama nasi tutakuja kupata barabara wala umeme lakini sasa umekuja hivyo hii ni neema ya pekee kwetu wananchi wa huku"Alisema Izengo
Aidha amemtaka Mbunge kutokubweteka na sifa anazopewa na wananchi bali aongeze bidii za kuwatumikia wananchi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Simon Songe amempongeza Diwani huyo kwa kuwa mstali wa mbele katika kusimamia maendeleo kupitia fedha zinazotolewa na serikali
Aidha Mhe Songe amewataka wasimamizi na wajenzi wote katika miradi mbalimbali kuongeza speed ya ujenzi ili miradi hiyo iweze kuanza kufanya kazi kama ilivyokuwa imekusudiwa.
"Nitaendelea kuwasemea Bungeni ili serikali yetu chini ya Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan ituletee maendeleo katika Jimbo letu la Bundle "Alisema Songe
MWISHO



0 Comments