WAZEE WAMTABILIA MAKUBWA SONGE.

Na Shushu Joel,Busega.

WAZEE wa kata ya Mwamanyili wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wamamtabilia mambo makubwa Mbunge wa Jimbo la Busega Mhe. Simon Songe kutokana na mwenendo wake wa uchapaji wa kazi ndani ya jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu Simon Songe akisalimiana na moja na wazee


Wakizungumza kwa wakati tofauti tofauti kwenye kwenye kikao cha hadhara kilichofanyika katika kijiji cha Nyasho"A" kata ya Mwamanuili .

Daniel Ngw'andu alisema kuwa katika jimbo hili wamepita viongozi wetu tangu kuanzishwa kwake lakini Mhe. Songe anaonekana ni kijana mpenda maendeleo na asiye na janja janja kama walivyokuwa watangulizi wake.


"Busega limekuwa Jimbo tangu mwaka 2000 na viongozi waliopita ni Ernes Nyanda,Dr Chegeni ,Dr Kamani na sasa ni Mhe Songe mwenye uchungu mkubwa na jimbo letu" Alisema.


Aidha aliongeza kuwa Mbunge Songe amekuwa akifuatilia zaidi maendeleo ya wananchi tofauti sana na kipindi cha viongozi wengine waliopita katika jimbo letu.


Naye Witness Masangu(57) alisema kuwa kijana huyu anaonekana kuwa ni nguzo kubwa kwa wananchi wa jimbo zima kwani muda mchache tu tangu achaguliwe kuwa mbunge amekuwa akijitoa kwa hali ya juu kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa haraka ndani ya jimbo la Busega.


Baadhi ya wazee wakimsikiliza mbee ibnahamu ili kupata elimu

"Kijiji chetu kilikuwa na uhaba mkubwa wa maji kwa kipindi kirefu lakini siku chache tu za uongozi wake maji yameanza kutoka tena bila kikoma"Alisema Witness


Naye Diwani wa kata hiyo Timoth Mayala amewapongeza wazee hao kwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Mhe. Mbunge Songe.


Aidha Mayala amewataka wazee wa kata yake kuendelea kumuombea mbunge ili azidi kuwatumikia.


Naye Mbunge alisema kuwa wananchi ndio wanaojua kipimo cha viongozi wanaofanya vizuri katika uongozi.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments