AFISA MIPANGO CHALINZE ATOA USHAURI CHANJO YA CORONA

Na Shushu Joel,Chalinze.

AFISA Mipango wa halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Shabani Milao amewataka wananchi wote nchini kupuuza maneno ya upotoshaji yanayotelewa na baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa letu.

Afisa mipango wa chalinze Ndugu Shabani Milao akichoma chanjo ya CORONA(NA SHUSHU JOEL)

Ushauri huo ameutoa mara baada ya kupatiwa chanjo ya ugonjwa wa Corona.

Akizungumza mara baada ya tukio hilo Milao alisema kuwa kumekuwa na upotoshaji wa hali ya juu kupitia kwenye mitandao ya kijamii hivyo ni bora ikapuuziwa.

"Hakuna mtu mwenye nia mbaya na na watanzania hivyo tujitokeze kuchoma chanjo ili tuwe salama"Alisema

Aidha Milao aliongeza kuwa chanjo zimekuwepo miaka mingi na hata enzi zao walidanganywa sana juu ya chanjo mbalimbali lakini mpaka leo wapo hai na Afya ziko salama.

Aliongeza kuwa ni vyema vijana wenzangu wakajitokeza kwa wingi maana wao ndio tegemeo la taifa  letu hapo kesho hivyo ni bora wakapata chanjo hizi kwa ajili ya usalama wa afya zao.

Naye mtaalam wa Afya kutoka halmashauri hiyo ya chalinze Beatha Mchopa alisema kuwa chanjo ni salama na ni muhimu kwa Afya zetu.

Hivyo niwashauri watu wote kujitokeza kupata chanjo ambazo zimekuwa zikiendelea kutolewa kote nchini kwa ajili ya ulinzi wa miili yetu.

Aidha Mchopa ameipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuwapambania wananchi wake kupata chanjo kwani ni muhimu kwa kwa afya zetu.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments