Na Shushu Joel, Busega.
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu umesifu mwenendo wa usukumaji wa maendeleo kwa wananchi wa Jimbo hilo ambao unafanywa na Mbunge wao Mhe Simon Songe.
![]() |
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Donald Deus katikati akiendesha kikao cha umoja wa vijana(NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza katika baraza la Umoja huo Mwenyekiti wa jumiuya hiyo Donaid Deus alisema kuwa tangu kuapishwa kwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mbunge wa Busega amekuwa ni kiongozi wa pekee kutokana na kuwa mstali wa mbele katika kufuatilia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
"Kwa kweli hatua ambazo amekuwa akizifanya Mhe Mbunge Songe kwa wananchi ndio ambazo zinahitajika kufanyika kwa viongozi"Alisema Deus
Aidha aliongeza kuwa viongozi wa namna ya Songe wamekuwa wakikisaidia chama cha Mapinduzi(CCM) kujielezea kwa wananchi kutokana na utekelezaji wa Ilani ambayo ndio kipaumbele cha chama kwa jamii .
Mbali na hilo Mwenyekiti huyo amewataka Vijana wa Jimbo la Busega kutembea kifua mbele kutokana na muda mchache wa uongozi wa Mhe Songe lakini utekelezaji umekuwa ni mkubwa na unazidi kwenda kwa kasi kila kata.
Kwa upande wake katibu wa Vijana wa kata ya Kiloleli Kusekwa Sjjaona amesema kuwa kweli Mbunge Songe amekuwa kimbilio kwa vijana mbalimbali wa wilaya na hasa kwenye nyanja ya ushauri wa kisiasa,uchumi na kijamii.
Hivyo amewataka vijana wenzake kuhakikisha wanazidi kumuunga mkono kwani yajayo yanafurahisha.
Naye Jesca Babasha amepongeza juhudi zinzofanywa na Mbunge kwa wananchi wa Jimbo la Busega kwa kuhakikisha wanapatiwa mahitaji muhimu ya maendeleo ikiwemo maji,umeme na mabalabala kitu ambacho awali kulikuwa ni historia kwao.
Aidha amewataka viongozi na wana CCM kuhakikisha wanaikumbatia tunu hiyo ambayo inatokea mara moja sana katika jamii.
MWISHO
0 Comments