MWAKAMO AKABIDHI VITAMBULISHO WAZEE.

 

Na Shushu Joel,Kibaha Vijijini

MBUNGE wa Kibaha Vijijini Michael Mwakamo amefanikiwa kukamilisha ahadi yake ya kuwatengenezea vitambulisho vya matibabu wazee katika jimbo hilo ili kuondokana na changamoto iliyokuwa ikiwakabili awali.

Mbunge wa jimbo la kibaha vijijini Mhe:Michael Mwakamo akimkabidhi kitambulisho mmoja wa wazee kwa ajili ya matibabu.

Akizungumza wakati wa utoaji wa vitambulisho hivyo Mwakamo amewataka wazee kuhakikisha wanavitumia vitambulisho hivyo kama ilivyokusudiwani kwani dhamira yake ni kuwaondolea wazee hao kupanga panga foleni pindi wanapokwenda kupatiwa matibabu.

 

“Sitaki kuona mzee yeyote Yule ndani ya jimbo hili kuona anateseka na matibabu ndio maana nimeamua kutoa pesa yangu ili kufanikisha zoezi la nyie kupatiwa huduma bure”Alisema Mwakamo

Baadhi ya wazee wakimsikiliza mbunge wakati akihutubia kabla ya kuwakabiidhi vitambulisho vya matibabu bure.

Aidha aliongeza kuwa endapo ikitokea mzee anapatiwa manyanyaso ya aina yeyote ile katika shughuli za huduma za basi mtu huyo anayefanya hivyo hatakuwa hajielewi maana naye ni mzee mtarajiwa.

 

“Leo tumewakabidhi vitambulisho vya matibabu wazee 209 wa kata ya Ruvu tu ingawa bado wataalamu wanaendelea na utengeneaji wa kata nyingine lengo lengu ni kuwakabidhi wazee wote wa jimbo waoatao 500 hivyo huu ni mwanzo tu nitaendelea kila kata mara tu idadi ya kata Fulani inapokamilika”Alisema Mwakamo.

Naye mmoja wa wanufaika wa vitambulisho hivyo Ndugu Adam Panjinga amempongeza mh Mbunge kwa msaada mkubwa alioutoa kwa wazee wa jimbo hilo ambao walipata shida juu ya kupata huduma za Afya.

 

Aidha aliongeza kuwa jambo hilo la kupata huduma za matibabu kwa kutumia vitambulisho vya uzee.

 

“Jambo hilo utolewa na serikali lakini kwa jimbo letu mbunge wetu ameamua kujitolea ili wazee wake tuweze kuondokana na changamoto ya matibabu kwenye sehemu za utoaji wa huduma za Afya”Alisema.

 

Naye Mganga mkuu wa mlandizi Dr Ibrahim Isack ametumia muda huo kuwataka waganga wafawidhi kwenye vituo vyote ndani ya wilaya hiyo kuhakikisha wanawapatia kipaumbele wazee wote wanaofika kwenye vituo vya Afya kwa ajili ya matibabu.

 

MWISHO

Post a Comment

0 Comments