Na Shushu Joel,Miono.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Ndg Makota Mkwayu amewataka Vijana wa wilaya hiyo kuweza kutumia vipaji vyao ili kujiongezea kipato.
![]() |
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Bagamoyo Makota Mkwayu akisisitiza jambo kwa vijana waliojitokeza kwenye kikao hicho(NA SHUSHU JOEL) |
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya vijana.
Aliongeza kuwa kijana unapotumia fursa ya kipaji chako unakuwa na nafasi Kubwa ya kujiongezea kipato chako na pia unatengeneza uaminifu mkubwa kwa jamii inayokuzunguka.
"Vijana wenzangu tunatakiwa kufikilia nje ya boksi kwani tumekuwa wazenbe wa kutumia vipaji vyetu ambavyo tumebarikiwa na Mungu hivyo sasa vijana tuamke na tutumie vipaji vyetu" Alisema Mkwayu .
Aidha ameiomba serikali kuendelea kuwapa nafasi kama inavyofanya sasa kwa kuwapatia nafasi za uongozi ili kusaidia taifa let.
Naye Mwajuma Ally amempongeza Mwenyekiti huyo wa vijana kwa maono yake ya mbali na jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa vijana wenzake.
Hivyo amemtaka kuendelea kuwa na tabia hiyo ya ushauri kwa vijana kwani ndio tegemeo la Taifa katika utendaji wa shughuli mbalimbali.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ya Miono Juma Mpwimbwi amewataka vijana kuendelea kuwa na umoja ili kujenga nchi yetu ambayo imekuwa ni mfano mkubwa wa kuigwa kwa mataifa mbalimbali.
MWISHO
0 Comments