SONGE AZIDI KUIPAISHA BUSEGA KIMAENDELEO

Na Shushu Joel,Busega.

MBUNGE wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu Mhe. Simon Songe amefanikiwa kuwakata kiu ya muda mrefu iliyokuwa ikiwasumbua wananchi wa jimbo hilo.

Mbunge wa jimbo la Busega Mkoani Simiyu Mh: Simon Songe akisisitiza jambo mbele ya wananchi katika moja ya mikutano yake(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamigongwa kata ya Malili katika moja ya ziara zake Mhe Songe aliwaambia wananchi hao kuwa kilio chao cha barabara ya kutoka malili kwenda Mwamigongwa mpaka mkula sasa inakwenda kutatuliwa ili wananchi wa maeneo hayo waweze kutengeneza uchumi kwa kujiongezea kipato kutokana na urahisi wa usafiri.

"Ndoto yangu siku moja ilikuwa kuona wananchi wa jimbo langu wanaenda kunufaika kupitia mazao yao wanayoyalima lakini kwa uwepo wa usafiri wa uhakika"Alisema Songe.

Aidha aliongeza kuwa kwa sasa pesa ipo na mkandarasi tayari yupo site na anaendelea na baadhi ya kazi kama ujenzi wa makalavati hivyo niwaombe wananchi wangu kutumia vizuri miundombinu hiyo ili itusaidie katika kukuza uchumi wetu  wa wanabusega. 

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Malili Christopher Bukalasha amemsifu mbunge na kudai kuwa amekuja kuwa ni mkombozi wa wananchi wa kata yangu kwani kijiji cha Mwamigongwa kilikuwa kama kipo kisiwani kutokana na ukosekanaji wa barabara kwa kipindi kirefu.

Pia amemsifu kwa kuonekana kuwa na uchu wa maendeleo kwenye jimbo letu la Busega ambalo lilikuwa likichezewa tu na baadhi ya wanasiasa ambao wamekwisha kupita kama viongozi. 

Ngw'ashi Masangu amemsifu Mbunge Mhe Songe kwa jinsi ambavyo amekuwa akijitoa kwa wananchi wake kwa kuwafanikishia ndoto zao ambazo zilikuwa zikihitajika kwa muda mrefu.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments