DED MGONJA AFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI MKURANGA.

Na Shushu Joel

MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani  Bi'Mwantum Mgonja  amewafungulia wawekezaji wa ndani ya Tanzania na wale wa  nje ya mipaka ya Tanzania kuweza kuja na kuwekeza katika wilaya hiyo.

Mkurugenzi wa wilaya ya Mkuranga Bi,Mwantum Mgonja katikati akisikiliza jambo kwa makini(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza na waandishi wa habari Ngoja alisema kuwa wilaya ya Mkuranga ila kila ajna ya mali Ghafi za kuwafanya wawekezaji kumiminika katika wilaya hiyo.

"Mkuranga ina Ardhi ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo njooni muwekeze sie tuko tayari kwa ajili yenu"Alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha Ngoja aliongeza kuwa kumiminika kwa wawekezaji katika wilaya ya Mkuranga kutatuongezea ukusanyaji wa mapato na pia kutengeneza ajira nyingi kwa wakazi wa Mkuranga.

Aliongeza kuwa wilaya ya Mkuranga imejipanga katika kuhakikisha kuwa kila mwekeza anapata kile anachokihitaji na hasa ulinzi wa mali zao.

Kwa upande Shabani Manda Diwani wa kata ya Tengelea amempongeza Mkurugenzi huyo kwa kufungua milango kwa wawekezaji kwa lengo la kujiongezea kipato kwa halmashauri yetu ya Mkuranga. 

Hivyo kuongezeka kwa wawekezaji katika wilaya yetu kutachochea maendeleo makubwa kutokana na ukusanyaji mkubwa wa fedha zitakazoenda kwenye miradi mbalimbali kwa jamii.

Naye Juma Sese ni Mkazi wa wilaya hiyo alisema kuwa kutokana na utendaji wa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Mkuranga naona wilaya yetu ikifika mbali mara baada ya ongezeko la wawekezaji. 

Aidha Sese aliongeza kuwa uwepo wa wawekezaji kutaongeza wingi wa ajira kwa wananchi pia pato kwa halmashauri na kingine kikubwa ni utekelezaji wa miradi kupitia fedha za ndani.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments