Na Shushu Joel,Rufiji.
WAZEE wa Chama Cha Mapindunzi(CCM) wa wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani wameupongeza uongozi wa Chama hicho kwa kuwaletea katibu mahiri,Msikivu na mpenda maendeleo.
![]() |
| Katibu wa CCM wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Omary Mtuwa |
Tangu wilaya yetu inaanzishwa hatujawai kuwa na kiongozi hodari na mpiga kazi kama Omary Mtuwa kwani kijana huyu amekuwa kiongozi wa pekee katika utendaji wake wa kazi za Chama.
Ally Ramadhani(79) mkazi wa Ikwiriri Alisema kuwa wilaya ya Rufiji imekuwa na viongozi wengi wa Chama ambao walipita kwa nyakati tofauti tofauti lakini katibu wa sasa ni kiongozi mwenye uchungu na Rufiji utafikili ni mkawa wa maeneo ya huku.
"Kusema kweli Mtuwa amekuwa akijituma sana kwenye utendaji wake kwani amefanikiwa kuifanya wilaya ya Rufiji kuwa na Umoja"Alisema Ramadhani.
Aidha Alisema kuwa ni mbaya kumsifia mtu lakini utendaji wa kijana huyu ni wa kuigwa sana katika Chama na nje ya Chama.
Kwa upande wake Bi' Fatma Nassoro(68) alisema kuwa wilaya ya Rufiji imekuwa na maendeleo makubwa ikilinganishwa na vipindi vilivyopita hii yote ni kutokana na uongozi imara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya katibu mwenye uchungu na maendeleo ya Rufiji Omary Mtuwa.
Aidha alisema kuwa kutokana na utendaji anaouonyesha katibu wa CCM huyo tunaamini atafika mbali katika uongozi wake na hasa katika usimamizi wa maendeleo ya Chama kwa wananchi.
Naye katibu wa ccm wilaya hiyo Omary Mtuwa mara baada ya kuzungumzwa na wazee hao alisema kuwa yeye ni wajibu wake kufanikisha usimamizi wa maendeleo unatekelezeka kama vile ulivyokusudiwa na serikali kupitia Chama.
Aidha aliongeza kuwa kuhusu utendaji wa kazi wananchi ndio wanaona hivyo mie najiona nipo kawaida tu .
"Tufanye kazi kwa weredi ili Chama chetu kiendelee kushika dola kwa usimamizi wa miradi mbalimbali ambayo imebainishwa ndani ya Ilani na ile ya ubunifu wetu viongozi" Alisema katibu Omary Mtuwa
MWISHO

0 Comments