Na Shushu Joel,Kibaha
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali walio katika mkoa huo wamekutana ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa kwa lengo la kutengeneza mikakati ya kufanya kazi za kuhakikisha mkoa huo unatangazika kutokana na upekee wa vitu vilivyo ndani ya mkoa wa Pwani.
![]() |
| Mkuu wa Pwani Abubakar Kunenge akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari(NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza
na wana hbari hao Kunenge alisema lkuwa Mkoa wetu umebalikiwa kuwa na kila kitu
ambacho mikoa mingine na hata nchi jirani hawana hivyo niwaombeni wana habari
kutumia taaluma yenu kuhakikisha mna wahabarisha wananchi ili waweze kujua kile
kilichopo ndani ya mkoa wao.
“Niwashukuru
kwa kuitikia wito huu kwani ni ngumu kuwapata waandishi wote na hii ni kutokana
na wingi wa kazi zenu lakini mmeitikia wito kweli naamini mmenipa heshima kubwa
sana mkuu wenu wa mkoa name sitowaangusha katika shughuli zenu za kila
siku”Alisema Mkuu wa Mkoa Kunenge.
Aidha
aliongeza kuwa mkoa wa Pwani una kila sababu ya kuwa namba moja kitaifa
kutokana na uwepo wa kila kitu katika Nyanja karibia zote.
Kwa upande
wake Mohamed Nandonde mwandishi wa
habari wa EATV amempongeza mkuu huyo wa Mkoa kwa kutambua thamani ya waandishi
na hata kuamua kufanya kikao kwa ajili ya kujadili jinsi gani mkoa wa Pwani
utakavyotangazwa na wana habari hao kupitia vyombo vyao vya habari.
Aidha
aliongeza kuwa ni kweli mkoa wa Pwani una kila sababu ya kuwa kinara katika
kila Nyanja kutokana na jinsi mkoa huo ulivyo jipambanua kwani viwanda ni
vingi,mazao meni mengi na kila kitu kipo kwenye mkoa huu wa Pwani.
Naye Monica
Samba ni mwandishi wa habari wa star Tv alisema kuwa ni vyema sasa kila
mwandishi akajipambanua na kutumia fursa iliyotolewa na mkuu huyo wa mkoa kwa
waandishi wote wa mkoa wa Pwani.
MWISHO

0 Comments