Na Shushu Joel,Busega.
MBUNGE wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu Mhe:Simon Songe amewataka wanafunzi kuchangamkia nafasi ya kusoma masomo ya sayansi kwa kusudi la kuja kulitumikia taifa letu kwa weredi wa hali ya juu.
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Busega Mh: Simon Songe akizungumza na waWanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Mkula(NA SHUSHU JOEL) |
Sayansi ni masomo mepesi sana kuliko masomo mengine na hasa somo la Hesabu pia ni masomo yenye kuhitajika sana kutokana na uchache wa watu waliosoma masomo hayo katika taifa letu na hasa kwenye kipindi chenu,hivyo niwaombeni kila mmoja wenu kuchangamkia fursa ya kusoma masomo ya sayansi
Aliongeza
kuwa serikali ya Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassani imejikita kwenye
kujenga maabara za aina tatu kwa kila shule ambazo ni biologia,kemia na physicia
kwa kusudi la kuwawezesha wanafunzi kutokupata changamoto ya aina yeyote ile
pindi mnapojifunza masomo hayo kwa vitendo.
“Someni
masomo ya sayansi kwani yana uharaka wa upatikanaji wa ajira hivyo hii ni fursa
kwenu wanafunzi wa Busega”Alisema Mhe: Songe
Aidha Songe
amewataka wanafunzi wote wa jimbo hilo kuhakikisha wanaongeza bidii katika
kujisomea kwani elimu ni mtaji wa elimu na elimu nzuri inaanzia hapa mlipo
sasa.
“Shule yetu
ya mkula imekuwa miongoni mwa shule kumi bora zilizofanya vizuri kwa wanafunzi
wa kidato cha sita hivyo na nyie mpambane muwazidi watangulizi wenu kwani sie
wazazi wenu furaha yetu ni kuona nyie mkifanya vizuri kwenye masomo
yenu”Alisema Songe.
Kwa upande
wake Mwajuma Ally ambaye ni mwanafunzi wa kitado cha sita amemwakikishia mbunge
kuwa wao wamejipanga kufanya vizuri zaidi ya watangulizi wao.
Pia wamempongeza mbunge kwa juhudi zake za kuhakikisha shule hiyo ya Mkula inakuwa na michepuo yote yaani sayansi na hati.
![]() |
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mkula wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Busega Simon Songe (NA SHUSHU jOEL) |
Naye Ngwashi
Ibrahimu ni miongoni mwa wanafunzi wa kidato cha tano waliochaguliwa mwaka huu
alisema kuwa Mhe: Songe ni mbunge wa pekee kwani ametufariji sana wanafunzi na
kututia moyo kwa ajili ya kusomo kwa bidii ili baadae kuja kulisaidia taifa
letu.
Aidha
aliongeza kuwa uwepo wa maabara kutafungua fursa kwa wanafunzi wote yaani wale
wa kidato cha kwanza mpaka cha nne kuweza kujifunza kwa vitendo na hata baadae
wale wa kidato cha tano na sita wakianza kusomo masomo hayo katika shule yetu
kutakuwa na wasomo wa pekee katika shule ya Mkula sekondari.
MWISHO
0 Comments