Katika kukabiliana na wimbi la tatu la Uviko 19 kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya World Logistics company (WLC, )imezindua huduma ya kusafirisha mizigo ili kumfikia mteja kwa urahisi ijulikanayo Cargo Pickup Delivery Service.
![]() |
Mkuu wa kitengo Cha masoko bi Agnes wa kwanza kushoto akizungumza na waandishi wa habari |
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha Masoko wa kampuni hiyo Agnes Daniel alisema kuwa huduma hiyo inatarajia kumuhakikishia Muagizaji na Mpokeaji kuepuka usumbufu na gharama za usafiri na zinginezo.
"Huduma hii itamsaidia anayeagiza mizigo kuepuka usumbufu nakuepuka gharama zinginezo nakubaki Salama dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19,. Alisema Agnes Daniel.
Agnes alisema kuwa kupitia teknojia Muagizaji ataweza kufuatilia mzigo wake katika hatua zote za usafirishaji za mizigo kuanzia siku yakwanzaalipoagiza Mzigo na kupokeamzigo huo kwa kutumia nyenzo ya Google Excle.
Aliongeza kuwa tofauti ya nyinginezo za usafiri shaji kampuni hiyo imejikita kufanya shughuli zake kupitia teknolojia hiyo.
MWISHO
0 Comments