UONGOZI MKOA WA PWANI WAZURU KUJIONEA MIRADI YA KIMKAKATI

Na Shushu Joel, Pwani


UONGOZI wa Mkoa wa Pwani ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Ndugu Abubakar Kunenge umetembelea miradi mikubwa miwili  iliyo ndani ya Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar kunenge akizungumza na wajumbe wa mkoa waliojitokeza kuangalia miradi ya maendeleo(NA SHUSHU JOEL)

Miradi iliyotembelewa na uongozi huo ni ule wa daraja lililopo katika halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo iliyogharimu serikalj kiasi cha shilingi Bilioni 72 na ule wa Treni ya kisasa (SGR) ambao nao umeigharimu serikali kiasi cha shilingi Trioni 2.

Akizungumza mbele ya timu hiyo kiongozi wa msafara huo ambaye ni Mkuu wa Mkoa Kunenge alisema kuwa kama timu ya uongozi wa Mkoa tumeamua kutembelea miradi hiyo kwa kusudi la kujionea pale ilipofikia na kujua lini sasa inakwenda kuanza kuwahudumia wananchi.

 "Uongozi umeambatana na wakuu wa wilaya wote,wakurugenzi wa halmashauri zote,makatibu tawala wilaya zote,wenyeviti wa halmashauri zote,viongozi wa usalama Mkoa na baadhi ya wakuu wa udara kutoka Mkoani "Alisema Kunenge.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa ni vyema sasa kila mtanzania akawa ni mlinzi wa miradi hii kwani serikali imetumia pesa nyingi kwa ujenzi wa miradi hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe:Ridhiwani Kikwete alisema kuwa daraja la mto   Wami ilikuwa ni kilio kikubwa kwa wananchi wa chalinze kwani wananchi walikuwa wakiteseka sana wakati wa daraja la awali kutokukidhi.

Lakini kutokana na usikivu wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tatizo hilo linaenda kubaki historia  kutokana na ujenzi wa daraja kubwa lenye mita 510 ambalo ni miongoni mwa madaraja  makubwa nchini na ya kisasa kabisa.

Hivyo Kikwete ameishukuru sana Serikalj kwa usikivu wa hali ya juu na hasa katika utekelezaji wa maendeleo kwa wananchi wake.

"Vijana zaidi ya 500  wa Jimbo la Chalinze wamepata ajira kutokana na uwepo wa mradi huo"Alisema Kikwete.

Naye Eng Tadeo Kamu ambaye ni msimamizi wa mradi wa Reli kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro alisema kuwa mradi huo mpaka sasa umekamklika kwa 93% na Treni hiyo itakuwa ni ya kisasa kabisa katika nchi yetu.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments