Na Shushu Joel,Pera.
DIWANI wa kata ya Pera iliyoko katika halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Mhe. Jackson Mkango ameanza ujenzi wa barabara ambazo zilikuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi wa kata hiyo.
Diwani wa kata ya Pera Jackson Mkango akiongoza shughuli za utoaji wa miti iliyopo njiani ili gari la kuchonga barabara liweze kuendelea na kazi zake(NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la ujenzi wa barabara ya kutokea kabululeni mpaka Genda,Mkango alisema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni kubwa na ilikuwa na uhitaji mkubwa wa kutengenezwa kutokana na wananchi wengi kutumia barabara hiyo.
"Barabara zinapotengenezwa zinasaidia kufunguka kwa mawasiliano hivyo mawasiliano yanapokuwa uchumi wa wananchi unaongezeka kwa kutokana na mwingiliano" Alisema Mkango .
Aidha Diwani huyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha wanachangamkia fursa ha uwepo wa barabara hiyo kwani vitu vingi vinakwenda kufunguka zikiwemo biashara za mazao.
Pia Mhe. Mkango amewataka wananchi kuwa walinzi wakuu wa miundombinu ambayo inatengenezwa kwa gharama kubwa ya pesa hivyo ni wajibu kila mmoja kuwa mlinzi.
Kwa upande wake Juma Ally(78) Mkazi wa Pera amempongeza Diwani huyo kwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo ilikuwa imesaulika kwa kipindi cha miaka mingi.
Aliongeza kuwa Barabara hiyo yenye kilometa zaidi ya sita itakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Pera kwa kufanya biashara.
Naye Khadija Athumani amempongeza Diwani huku akisema kuwa sasa Pera imepata kiongozi ambaye tulikuwa tukimuhitaji kuwa nae.
MWISHO
0 Comments