Na Shushu Joel,Kisarawe
JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Mkoa wa Pwani kimewata wanafunzi wa kike kuzingatia masomo na kuachana na tama zote za hapa duniani.
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ambaye pia ni Waziri wa Muungazo na Mazingira Seleman Jafo kulia sambamba na Faridi Mgomi wakiwakabidhi wanafunzi wa shule ya Kimani Sec zawadi (NA SHUSHU JOE)
Rai hiyo
imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Farida Mgomi alipokuwa akizungumza na wanafunzi
wa kidato cha nne,Tano na wale wa kidato cha sita katika shule ya sekondari
Kimani iliyoko wilaya ya Kisarawe.
Alisema kuwa
kumekuwa na tabia ya ajabu kwa wanafunzi wa kike kwa kutamani maisha ya watu
wazima kitu ambacho kimekuwa kikiwaghalimu sana katika kuendeleza masomo yao
kwa kutimiza ndoto zao.
“Bodaboda,chips,makondakta
na Vijana masharobalo ni watu ambao wamekuwa wakiwakatisha masomo watoto wa
kike kwa kuwadanganya danganya na vitu vidogo vidogo na hata wengine kufikia
hatua ya kuacha shule kwa upataji wa mimba”Alisema Mgomi.
Aidha katika
jumuiya hiyo imefanikiwa kutoa zawadi mbalimbali za mahitaji ya wanafunzi wote
walioko kambi ya kujiandaa na mtihani wa mwisho pia wametoa taulo za kike kwa
ajili ya wanafunzi ili kuweza kuwasaidi kwenye kambi hiyo.
Naye Mkuu wa shule katika shulje hiyo Hillary Bwagidu amewapongeza wanawake hao kwa zowadi lukuki walizozitoa kwa wanafunzi wa shule yake huku wakisema kuwa hii ni kama deni la kuhitaji ufaulu kwa watoto wetu.
Aidha alisema kuwa zawadi walizozipokea ni nyingi na tunaamini zitatusaidia mpaka tunamaliza mtihani wetu wa taifa na chakula hiki kitakuwepo tu kwani ni kingi sana
Kwa upande
wake Neema Ally mwanafunzi wa kidato cha nne amewashukuru wazazi hao kwa msaada mkubwa
waliokuwa wakihitaji kupata lakini sasa changamoto hiyo imekwenda kutatuliwa.
MWISHO
0 Comments