Na Shushu Joel, Kibaha.
MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Pwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bi' Subra Mgalu ametembelea kambi ya wanafunzi inayojiandaa na mtihani wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Nyumbu iliyoko wilaya ya kibaha Mkoani Pwani.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani Mhe:Subira Mgalu akiwakabidhi wanafunzi wa shule ya sekondari Nyumbu baadhi ya mahitaji ya kambi(NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza na wanafunzi hao Mhe: Mgalu amewataka wanafunzi hao kuzidi kuongeza bidii za kujisomea kwani bado wanayo nafasj ya kufanya vizuri kwenye mtihani wa Taifa ujao.
"Elimu ni ufunguo wa maisha hivyo ni vyema mkaongeza bidii za masomo ili mfaulu na kisha kuendelea na masomo ya vyuo ambayo yatafungua mwelekeo wa maisha yenu"Alisema Mgalu.
Aidha alisema kuwa naamini kambi hii lazima italeta mafanikio yanayohitajika kwenu na Wazazi kwa ujumla hivyo nawaunga mkono kambi yenu kwa kuwapatia chakula ambacho mtakitumia mpaka ambapo mtakapofunga kambi yenu ya maandalizi ya mtihani.
Mbali na misaada hiyo ya vyakula Mhe:Mgalu amewatahadbalisha wanafunzi wa kike kutokukukali kudanganyika na vijana walioko mtaani na kisha kuwaachisha masomo yao kwani Wazazi na walezi bado wanahitaji waweze kuhitimu masomo yao ili wafikie malengo yao.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Nyumbu Sekondari Ombeni Ally amemshukuru Mbunge huyo kwa misaada yake ya chakula kwa ajili ya wanafunzi hao walioko kambi hapo ambao wanatarajia kufanya mtihani wa kidato cha nne miezi michache ijayo.
Aidha Mkuu
huyo wa shule alisema kuwa kuna matumaini makubwa kwa wanafunzi waliopo kidato
cha nne na hii ni kutokana na maandalizi
yaliyofanyika na msaada mkubwa waliopatiwa wanafunzi hao na walimu wao.
"Msaada huu ulioutoa ni wa kutia moyo kwa wanafunzi wetu walioupokea hapa kambini hivyo endelea na moyo huo huo wa utoaji kwa jamii inayokuzunguka"Alisema Mwalimu Ally.
Naye Rose Mushi amempongeza Mhe: Subra Mgalu kwa misaada yake ya chakula aliyoitoa kwenye kambi hiyo huku akimwakikishia kuwa wanakwenda kufanya vizuri kwenye mtihani wao wa kidato cha nne.
MWISHO
0 Comments