Na Shushu Joel, Chanika.
MKURUGENZIA wa Chuo cha Afya na Sayansi shirikishi cha City Ndg Shabani Mwanga ameongoza jopo la wanafunzi wa chuo hicho kuchangia damu salama kwa kusudi la kuchangia damu hiyo katika vituo vya Afya na hospital zilizopo ndani ya wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa chuo cha City akisikiliza jambo toka kwa wanafunzi hayupo pichani(NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Mkurugenzi wa chuo hicho alisema kuwa ameamua kuchangia damu ili kuwasaidia wananchi wenye uhitaji ili kuweza kuokoa maisha yao.
Aliongeza kuwa zoezi hilo la uchangiaji wa damu limekuwa sambamba na sherehe za kutjmiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa kazi kwenye chuo cha City cha Ilala.
"Wanafunzu wangu wamenifurahisba kwa kuona umuhimu wa kujitolea kwenye zoezi la uchangiaji wa damu jambo ambalo limekuwa na changamoto kwa jamii kutojitokeza kwenye uchangiaji"Alisema Shabani Mwanga.
Pia Mkurugenzi Mwanga alisema kuwa unapotoa damu unawasaidia watu wengi wenye mahitaji kama vile Mama anapojifungua pia watu wanaopata ajali.
Mery Joseph ni Mwanafunzi wa mwaka wa pili kwenye nafasi ya utabibu amempongeza Mkurugenzi huyo kwa kuwa kiongozi wa pekee kwa wananchi na walimu kutokana na kuwa kiongozi huyo amekuwa akituchukulia kama wanae Ola kubwa amekuwa akisisitiza juu ya malili.
MWISHO
0 Comments