Na Shushu Joel,Chalinze
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Mhe Ridhiwani Kikwete amefanikiwa kutatua changamoto zilizowashinda watangulizi wake kwa kufanikiwa kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama iliyokuwa ni sugu kwenye Jimbo hilo.
| Mbunge wa jimbo la chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akifafanua jambo Bungeni(NA SHUSHU JOEL) |
Changamoto ya maji katika katika Jimbo la Chalinze ilionekana kuwa ni donda lisilitibika kwa kipindi cha uongozi mbalimbali uliopita katika Jimbo hilo.
Akizungumza kwa mara ya kwanza mara baada ya uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji katika Jimbo hilo Mbunge huyo (Mhe.) Ridhiwani Kikwete) alisema kuwa nimekuwa msumbufu kwa viongozi wa maji hapa nchini lengo langu ilikuwa ni kujua ni lini serikali itaenda kuondoa tatizo hilo kwa wananchi wa Chalinze ambao wamekuwa wakisikia tu kuna maji yatakuja.
"Binafsi ni jambo la kujivunia kwangu kwani ni hatua kubwa imefanyika kwa serikali dhidi ya wananchi wa Chalinze kwa kufanikisha upatikanaji wa huduma ya maji"Alisema Mbunge Kikwete.
Aidha aliongeza kuwa zile ndoto ambazo zilikuwa kwenye masikio yetu sasa zimetimia baada ya kukabidhiwa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi Bilioni 19 na mradi huo utakuwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni 9.3.
Aidha alisema kuwa Jimbo la Chalinze limefanikiwa kuwa na viongozi wengi waliopita kama wawakilishi wa wananchi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini hakuna hata mmoja ambaye amefanikiwa kumaliza tatizo hii ya maji kwa wakazi wao.
| Baadhi ya mafundi wa mtambo wa maji wakikamilisha ufungaji wa mitambo hiyo tayari kwa kuanza kazi.(SHUSHU JOEL) |
Wawakilishi waliofanikiwa kuongoza katika Jimbo la Chalinze kuanzia mwaka 1961- 1965 Dosa Azizi, 1965- 1970 Bakari Mgaza, 1970- 1975 Steven Pilla, 1975- 1980 Adrian Mpande, 1980- 1985 Leon's Semindu, 1985-1990 Kanali Yuseeph Baruti Ramiya hawa wote walikuwa wabunge wa Bagamoyo na Chalinze kabla ya kutenganishwa,1990- 2005 Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye Mbunge wa kwanza wa Jimbo la Chalinze,2005- 2010 Ramadhani Maneno,2010 - 2015 Said Bwanamdogo ambaye alifariki dunia na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge aliyepo madaraka Mhe Ridhiwani Kikwete ambaye ameonekana kuwa ni shujaa kwa wananchi wa Jimbo hilo kutokana na ushujaa wake wa kuutafuna mfupa wa changamoto ya maji Chalinze.
Akitoa shukrani mara baada ya uzinduzi wa mradi huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ramadhani Maneno alisema kuwa tatizo la maji lilikuwa ni sugu katika Jimbo la Chalinze lakini sasa limebakia ni historia hivyo kama Chama tunampongeza Mbunge wa Jimbo Mhe Ridhiwani Kikwete kwa utekelezaji mkubwa wa Ilani ya Chama kwani amewatua kinamama ndoo kichwani.
Aidha Mwenuekiti huyo aliongeza kuwa maji ni uhai hivyo upatikanaji wake kwa wananchi ni jambo njema na lenye faraja kwa serikali yetu .
Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso alisema kuwa pesa zote zilizokamklisha mradi huu ni za ndani hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuwa mlinzi wa mwenzake juu ya miundombinu .
Aidha amewapongeza wananchi wa Jimbo la Chalinze kuwa walichagua kiongozi mwenye uchu wa maendeleo na watu wake kwani amekuwa akifika mara kwa mara ofisi kwangu huku kilio chake kikiwa ni lini wananchi wangu wanapata maji na leo jambo hilo limekamilika kweli Kikwete ni kiongozi wa pekee.
MWISHO
0 Comments