Julieth Ngarabali, Kibaha
Baadhi ya kina Baba na kina Mama wakishirikiana kufanya usafi kwenye eneo linalotarajiwa kujengwa kituo cha Afya. |
Wakina baba wametakiwa kutambua changamoto wanazozipitia wake zao katika malezi ya watoto na kisha washirikiane kuzipatia uvumbuzi pamoja na kujenga tabia ya kuwathamini wasaidizi wao hao.
Akizungumza na wananncbi wa mtaa wa Mualakani, Balozi wa eneo hilo Msee Shekwamba amesema wakina baba wana mchango mkubwa katika kuhakikisha watoto wanapata huduma muhimu ikiwemo za afya, elimu , chakula na ulinzi muda wote na kuwaachia jukumu hilo wake zao pekee.
Aidha ametoa wito kwa wababa wote kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanashirikiana na wake zao katika majukumu mbalimbali ili kujenga familia na jamii Bora zaidi
"Pia akibababa jamani muwe mstari wa mbele kutetea haki za wanawake na watoto ili kuepuka ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa wanawake na watoto ambapo hupelekea majeraha makubwa ikiwa ni pamoja ulemavu wakudumu na kupoteza uhai"amesema
Awali wakina mama wa eneo hili wamataja baadhi ya matukio ya ukatili kuwa yanaunganishwa na Mila na desturi zisizofaa ama zilizopitwa na wakati ambazp bado jamii na hasa wanaune wanazitumia katika malezi ya familia.
Mmoja wa wanawake hao Hawa Saidi ameomba viongozi wa jadi na Dini kubeba jukumu la kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuachana nazo mika hizo kwani zinawaumiza wanawake na watoto.
"Pia wamehimiza wanaume kupima afya zao mara kwa mara ili kilinda familia zao na maradhi mbalimbali ikiwemo ya virusi vya Ukimwi"amesema Amina Taabu.
Awali Diwani wa kata ya Picha ya Ndege Karim Mtambo amewataka wanawake kutoa taarifa Mara moja Kwenye vyombo husika pale wanapofanyiwa matendo ya ukatili
Mwisho.
0 Comments